Miaka mia mbili iliyopita, katika asubuhi nzuri ya majira ya kuchipua mnamo mwaka 1820, kijana Joseph Smith, akitafuta kujua kanisa lipi ajiunge nalo, alikwenda msituni kuomba karibu na nyumba yake huko Kaskazini ya New York, Marekani. Alikuwa na maswali kuhusu wokovu wa nafsi yake na aliamini kwamba Mungu angemwongoza.