“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132: ‘Kama Tunapata Baraka Yoyote Kutoka kwa Mungu, Ni kutokana na Utii’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Novemba 8–14
Mafundisho na Maagano 129–132
“Kama Tunapata Baraka Yoyote Kutoka kwa Mungu, Ni kutokana na Utii”
Sehemu ya 129–32 inafundisha kanuni nyingi za thamani, chache tu kati ya hizo zimesisitizwa katika muhtasari huu. Ni kweli zipi nyingine unazozipata?
Andika Misukumo Yako
Brigham Young wakati fulani alisema juu ya Joseph Smith, “Angeweza kupunguza vitu vya mbinguni kwa uelewa wenye kikomo” (katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 499–500). Hii inaonekana kweli hususani juu ya mafundisho ya Nabii huko Nauvoo katika miaka ya 1840, baadhi yake yameandikwa katika Mafundisho na Maagano 129–32. Mwokozi yukoje? “Yeye ni mtu kama sisi.” Mbinguni kukoje? “Ujamaa ule uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule” (Mafundisho na Maagano 130:1–2), na mahusiano yetu ya kifamilia tuliyoyaenzi sana katika ulimwengu huu, kama yaliunganishwa kwa mamlaka sahihi, “yatakuwa na nguvu kamili” katika ulimwengu ujao (Mafundisho na Maagano 132:19). Kweli kama hizi zinaweza kufanya mbinguni kusiwe mbali sana—kutukufu, na bado kunafikika.
Lakini tena, wakati mwingine Mungu anaweza kututaka kufanya vitu ambavyo havileti faraja kabisa ambavyo vinaweza kuonekana haviwezi kufikiwa. Kwa Watakatifu wengi wa mwanzo, ndoa ya mitala ilikuwa moja ya amri. Amri ya kuoa wake wa ziada ilikuwa ni jaribu kali la imani kwa Joseph Smith, mke wake Emma, na karibia kila mmoja aliyeipokea. Kuweza kupita jaribu hili, walihitaji zaidi ya hisia zenye kufaa kuhusu injili ya urejesho; walihitaji imani kwa Mungu ambayo ilikwenda mbali zaidi ya matamanio au mapendeleo binafsi. Amri haipo tena leo, lakini mfano wa uaminifu wa wale walioiishi bado upo. Na mfano huo unatutia moyo tunapotakiwa kufanya “dhabihu zetu wenyewe katika utii” (Mafundisho na Maagano 132:50).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
Joseph Smith alifunua kweli kuhusu Uungu na “ulimwengu ujao.”
Unaweza kuona kwamba sehemu ya 130–31 inasomeka kitofauti kidogo kuliko sehemu zingine katika Mafundisho na Maagano. Hii ni kwa sababu sehemu ya 130–31 msingi wake ni kutoka kumbukumbu ambazo William Clayton, mmoja wa makatibu wa Joseph Smith, alitunza vitu alivyomsikia Nabii akifundisha. Matokeo yake, sehemu hizi ni zaidi kama mikusanyiko ya kweli badala ya ufunuo ulioambatana, uliotolewa imla. Hata hivyo, kuna baadhi ya dhima zinazofanana miongoni mwa kweli hizi nyingi. Kwa mfano, unaweza kusoma sehemu ya 130–131 ukiwa na maswali kama haya akilini: Ninajifunza nini kuhusu Mungu? Ninajifunza nini kuhusu maisha baada ya mauti? Ni kwa jinsi gani uelewa huu unaathiri maisha yangu?
Ona pia “Mioyo Yetu Ilishangilia Kumsikia Yeye Akiongea,” Ufunuo katika Muktadha, 277–80.
Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:7, 13–25
Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja milele.
Moja ya kweli za faraja mno zilizorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith ni kwamba mahusiano ya ndoa na familia yanaweza kudumu milele. Kupitia Joseph Smith, Bwana alirejesha ibada na mamlaka yaliyohitajika kufanya mahusiano haya yawe ya milele (ona Mafundisho na Maagano 132:7, 18–19). Fikiria kuhusu mahusiano ya familia uliyonayo au unayotumaini kuwa nayo hapo baadaye unaposoma Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:7, 13–15. Ni kwa jinsi gani mistari hii inaathiri jinsi unavyofikiri kuhusu mahusiano haya?
Wakati mwingine, hata hivyo, kanuni ya familia za milele sio ya kufariji—inaweza kuleta wasiwasi, hata huzuni, wakati hali za familia zetu za sasa hazifikii ukamilifu wa selestia. Wakati Rais Henry B. Eyring alipokuwa na mashaka kuhusu hali kama hiyo katika familia yake, alipokea ushauri huu wa hekima kutoka kwa mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Wewe ishi tu kwa kustahili ufalme wa selestia, na mipangilio ya familia itakuwa mizuri ajabu kuliko unavyofikiria” (katika “A Home Where the Spirit of the Lord Dwells,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 25). Ni jinsi gani kufuata ushauri huu kutakubariki katika hali ya familia yako kwa sasa?
Ona pia Kristen M. Oaks, “To the Singles of the Church” (Church Educational System devotional for young adults, Sept.11, 2011), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org.
Mafundisho na Maagano 132:1–2, 29–40.
Ndoa ya wake wengi inakubalika kwa Mungu iwapo tu Yeye mwenyewe ameamuru.
Yeyote ambaye amesoma Agano la Kale bila shaka alistaajabu kuhusu Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Musa, na wengine wakioa wake wengi. Je, wanaume hawa wema walikuwa wakifanya uzinzi? Au je, Mungu aliafiki matendo yao? Tafuta majibu katika Mafundisho na Maagano 132:1–2, 29–40.
Ndoa kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ni kiwango cha Mungu cha ndoa (ona kichwa cha habari cha sehemu kwenye Tamko rasmi 1; ona pia Yakobo 2:27–30). Hata hivyo, kumekuwa na vipindi katika historia wakati Mungu alikuwa ameamru watoto Wake kuwa na ndoa ya mitala.
Miaka ya mwanzo ya Kanisa la urejesho ilikuwa moja ya vipindi hivyo vya kipekee. Baada ya kupokea amri hii, Joseph Smith na Watakatifu wengine wa siku za Mwisho walikuwa na ndoa za mitala. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu ndoa ya mitala miongoni mwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa hapo mwanzo, ona “Mercy Thompson na Ufunuo juu ya Ndoa” (Ufunuo katika Muktadha, 281–93); Saints, 1:290–92, 432–35, 482–92, 502–4; “Plural Marriage in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org); “Why Was It Necessary for Joseph Smith and Others to Practice Polygamy?” (video, ChurchofJesusChrist.org).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani
-
Mafundisho na Maagano 130:2, 18–19; 132:13, 19.Unawezaje kuitumia mistari hii ili kuisaidia familia yako kuvipa kipaumbele vitu ambavyo vinadumu milele? Pengine ungeweza kupaki sanduku lako au begi la mgongoni kwa vitu vinavyowakilisha vitu ambavyo, kulingana na Mafundisho na Maagano 130:2, 18–19; 132:19, tunaweza kuchukua pamoja nasi kwenye maisha yajayo, kama vile picha za familia au maandiko. Ni nini Mafundisho na Maagano 132:13 inatufundisha kuhusu vitu vya ulimwengu? Hii inaweza kuelekeza majadiliano kuhusu kufokasi kwenye vitu ambavyo vina umuhimu wa milele.
-
Mafundisho na Maagano 130:20–21.Mnaweza kuimba wimbo kuhusu shukrani, kama vile “Hesabu Baraka Zako” (Nyimbo za Kanisa, na. 241), na kutengeneza orodha ya baraka ambazo familia yako imezipokea kwa kutii sheria za Mungu. Ni baraka gani tunatumaini kuzipokea? Tunawezaje kupokea baraka hizo?
-
Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:15–19.Video “Marriage Is Sacred” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kusaidia familia yako kujadili kweli katika mistari hii. Je, Bwana anahisi vipi kuhusu ndoa? Ni jinsi gani sisi—iwe tumeoa au tumeolewa au mseja—tunajiandaa kuwa na ndoa ya milele?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,188.