Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134: “Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi”


“Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134: ‘Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 15–21. Mafundisho na Maagano 133–134,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
wanawali watano wenye busara

Bwana harusi Anakuja, na Elizabeth Gibbons

Novemba 15–21

Mafundisho na Maagano 133–134

“Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi”

Rais Henry B. Eyring alifundisha: “Urejesho wa injili ulianza kwa swali la unyenyekevu lililotafakariwa katika nyumba ya kinyenyekevu, na unaweza kuendelea katika kila nyumba zetu” (“Nyumba Ambayo Roho wa Bwana Anaishi,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 25).

Andika Misukumo Yako

Wakati Kanisa lilipokuwa takribani miezi 19, Nabii Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa walipanga mipango yenye nia ya kukusanya funuo za Mungu za siku za mwisho katika juzuu moja na kuchapisha nakala 10,000—mara mbili ya chapisho la kwanza la Kitabu cha Mormoni. Kwa bahati mbaya, gharama kubwa iliingilia mipango hii, na majambazi walishambulia mtambo wa kupigia chapa wa Kanisa wakati uchapishaji unaendelea. Walitawanya kurasa zilizokuwa hazijafungwa, na ingawa Watakatifu shupavu walihifadhi baadhi yake, hakuna nakala kamili za Kitabu cha Amri zinazojulikana kuwa zilisalia.

Kile tunachojua sasa kama sehemu ya 133 ya Mafundisho na Maagano ilitakiwa kuwa ni kiambatisho kwenye Kitabu cha Amri, kama mahali pa mshangao mwishoni mwa ufunuo uliochapishwa wa Bwana. Inaonya juu ya siku ijayo ya hukumu na inarudia wito unaopatikana katika ufunuo wote wa siku za leo: kimbia ya ulimwengu, kama ilivyoashiriwa na Babilonia; jenga Sayuni; jiandae kwa ajili ya Ujio wa Pili; na sambaza ujumbe huu “kwa kila taifa, na kabila, na ndimi, na watu” (mstari wa 37). Wakati mipango ya mwanzo kwa ajili ya Kitabu cha Amri haikuweza kukamilishwa, ufunuo huu ni ukumbusho na ushahidi kwamba kazi ya Bwana haiwezi kuzuiwa, “kwani atauweka wazi mkono wake mtakatifu … , na miisho yote ya dunia itauona wokovu wa Mungu wao” (mstari wa 3).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 133

Kweli katika Mafundisho na Maagano zinaweza kuniandaa kufanya kazi ya Mungu.

Vitabu wakati mwingine vinaishia kwa hitimisho ambalo linatamka au kufanya muhtasari wa hoja kuu za kitabu. Sehemu ya 133 kiuhalisia ilikuwa imekusudiwa kuwa hitimisho la Kitabu cha Amri, na inaweza kuwa yenye thamani kusoma sehemu hii ukiwa na hilo akilini. Ni hoja zipi Bwana anazisisitiza kuhusu kazi Yake? Mistari ya 57–62 inakufundisha nini kuhusu jukumu ambalo Bwana anakutaka wewe ufanye katika kazi Yake?

Mafundisho na Maagano 133:1–19

Bwana ananitaka kujiandaa kwa ajili ya ujio Wake wa Pili.

Zote sehemu ya 1, dibaji ya Bwana kwenye Mafundisho na Maagano, na sehemu ya 133, kiambatisho cha kwanza kwenye Kitabu, zinaanza na ombi linalofanana kutoka kwa Bwana: “Sikilizeni, Enyi watu wa kanisa langu” (Mafundisho na Maagano 1:1; 133:1). Inamaanisha nini kusikiliza? (Ona Mwongozi kwenye Maandiko, “Sikiliza,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Ni mialiko gani au amri ambazo Bwana anakutaka wewe kusikiliza katika Mafundisho na Maagano 133:1–19? Ni niini kinakutia moyo wa kutenda ili kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya ujio Wake? Ni kwa jinsi gani utawasaidia wale wanaokuzunguka kujiandaa?

Ona pia Mathayo 25:1–13; D. Todd Christofferson, “Kujiandaa kwa ajili ya Kurudi kwa Bwana,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 81–84.

Mafundisho na Maagano 133:19–56

Ujio wa Pili utakuwa wa furaha kwa waadilifu.

Unaposoma katika Mafundisho na Maagano 133:19–32 kuhusu matukio ambayo yataambatana na Ujio wa Pili wa Mwokozi, unaweza kutafakari maelezo kuhusu matukio haya yanaashiria nini kwako kuhusu Mwokozi na kazi Yake. Ni yapi matumizi yamkini ya kiroho unayoweza kuyapata katika maelezo haya?

Unaposoma maelezo ya kurudi kwa Mwokozi katika mistari ya 32–56, ni nini kinakusababisha kuingojea siku ile iliyo kuu? Ni maneno gani au virai vinaelezea upendo wa Bwana kwa ajili ya watu Wake? Fikiria kuandika uzoefu wako binafsi wa “ukarimu wa Bwana [wako], na yote ambayo ameyaweka juu [yako] kulingana na wema wake” (mstari wa 52).

Mafundisho na Maagano 134

“Serikali zimewekwa na Mungu kwa manufaa ya mwanadamu.”

Mahusiano ya Watakatifu wa mwanzo na serikali yalikuwa magumu. Wakati Watakatifu walipolazimishwa kutoka Jackson County, Missouri, mnamo 1833, hawakupokea msaada wowote au fidia kutoka kwa serikali ya eneo hilo au serikali ya taifa licha ya maombi yao kwa ajili ya msaada. Wakati huo huo, baadhi ya watu nje ya Kanisa walitafsiri mafundisho kuhusu Sayuni kumaanisha kwamba Watakatifu walikataa mamlaka ya serikali za kidunia . Mafundisho na Maagano 134 iliandikwa, kwa sehemu, kufafanua msimamo wa Kanisa juu ya serikali.

Waumini wa Kanisa wanapaswa kuhisi vipi kuhusu serikali? Unapojifunza sehemu ya 134, fikiria kutengeneza orodha mbili: orodha moja ya kanuni unazojifunza kuhusu serikali na nyingine ya majukumu ya wananchi. Ni kwa jinsi gani mawazo haya yaliweza kuwa msaada kwa Watakatifu wa mwanzo? Ni kwa jinsi gani yanatumika pale unapoishi?

Ona pia Makala ya Imani 1:11–12; Mada za Injili, “Uhuru wa Dini,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 133:4–14.Kinyume cha Kiroho cha Sayuni ni Babilonia—jiji la kale ambalo katika maandiko yote linaashiria uovu na utumwa wa kiroho (ona D. Todd Christofferson, “Come to zion,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 37; Mwongozo kwenye maandiko, “Babeli, Babilonia,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Je, kuna chochote mnahitaji kufanya kama familia, katika hali ya kiroho, “kuondoka katika Babilonia” (mstari wa 5) na “kwenda …Sayuni”? (mstari wa 9).

Mafundisho na Maagano 133:20–33.Mnaposoma mistari hii pamoja, familia yako ingeweza kuchora picha ambazo wanafikiri Ujio wa Pili utavyokuwa. Mngeweza pia kucheza au kuimba wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83), na jadilini kile familia yako inachoweza kufanya kujiandaa kwa ajili ya Ujio Wake.

Mafundisho na Maagano 133:37–39.Je, familia yako ingefurahia kusoma mistari hii “kwa sauti kubwa”? (mstari wa 38). Inamaanisha nini kushiriki injili kwa sauti kubwa? Ni kweli zipi tunaweza kushiriki?

Mafundisho na Maagano 134:1–2.Ili kuisaidia familia yako kuelewa umuhimu wa serikali, ungeweza kujadili maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani familia yetu imebarikiwa kwa kuwa na sheria? Ni kwa jinsi gani nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na sheria? Ungeweza pia kutengeneza au kupaka rangi picha ya bendera ya nchi yako au kukariri makala ya imani ya kumi na moja na kumi na mbili.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Come, Ye Children of the Lord,” Nyimbo za Kanisa, na. 58

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Fundisha mafundisho ya wazi na rahisi. Bwana anaelezea injili Yake kwa maneno kama “uwazi” na “urahisi” (Mafundisho na Maagano 133:57). Maneno haya yanapendekeza nini kwako kuhusu kufundisha injili kwa familia yako?

Picha
Kristo katika joho jekundu

Kristo katika Joho Lake Jekundu, na Minerva Teichert

Chapisha