Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136: “Yeye ‘Ametia Muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe’”


“Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136: ‘Yeye “Ametia Muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe,”’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Gereza la Carthage kwa mwonekano wa nje

Gereza la Carthage

Novemba 22–28

Mafundisho na Maagano 135–136

Yeye “Ametia Muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe”

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 135–36, Bwana anaweza kukupa msukumo wa umaizi ili kukusaidia kutumia kile ulichosoma. Wakati hilo linapotokea, andika kile Anachokufundisha.

Andika Misukumo Yako

Adhuhuri ya Juni 27, 1844, iliwakuta Joseph na Hyrum Smith katika gereza kwa mara nyingine, wakiwa wameandamana na John Taylor na William Richards. Waliamini walikuwa hawana hatia ya kosa lolote, lakini walijisalimisha chini ya ulinzi, wakitegemea kuzuia machafuko dhidi ya Watakatifu waliokuwa Nauvoo. Hii haikuwa mara ya kwanza kwamba maadui wa Kanisa wamemuweka Nabii Joseph ndani ya gereza, lakini wakati huu alionekana kujua asingerudi akiwa hai. Yeye na rafiki zake walijaribu kufarijiana kwa kusoma kutoka katika Kitabu cha Mormoni na kuimba nyimbo za kanisa. Kisha milio ya risasi ilisikika, na ndani ya dakika chache maisha ya duniani ya Joseph Smith na kaka yake Hyrum yalifika mwisho.

Na bado haikuwa mwisho wa sababu tukufu waliyokuwa wameikumbatia. Na ilikuwa siyo mwisho wa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo. Kulikuwa na kazi zaidi ya kufanya na ufunuo zaidi ambao ungeliongoza Kanisa kusonga mbele. Kumuua Nabii kusingeweza kuua kazi ya Mungu.

Ona Saints, 1:521–52.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 135; 136:37–39

Joseph na Hyrum Smith walitia muhuri ushuhuda wao kwa damu yao.

Fikiria jinsi ambavyo ungeweza kuhisi kama ungekuwa unaishi Nauvoo wakati Joseph na Hyrum Smith walipouawa (ona Saints, 1:554–55). Ni kwa jinsi gani ungeweza kujaribu kuelewa tukio hili la majonzi? Mafundisho na Maagano 135, hapo awali ikichapishwa chini ya miezi mitatu baada ya kifo cha kishahidi, ingeweza kusaidia. Unaweza kuwekea alama maneno na virai ambavyo vingeweza kukuletea uelewa na uthibitisho. Ungesema nini kwa mtu fulani ambaye anauliza, “Kwa nini Mungu anaruhusu Nabii Wake auawe?”

Ona pia Mafundisho na Maagano 5:21–22; 6:29–30; “Kukumbuka Kifo cha Kishahidi,” Ufunuo katika Muktadha, 299–306; Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 522–23, 529–40; M. Russell Ballard, “Je, Hatupaswi Kusonga Mbele katika Kusudi Hili Kuu?Ensign au Liahona, Mei 2020, 8–11.

Mafundisho na Maagano 135:3

Joseph Smith amefanya mengi kwa ajili ya wokovu wetu zaidi ya yeyote mwingine isipokuwa Yesu Kristo.

Fikiri kuhusu baraka ambazo zimekuja kwako kama muumini wa Kanisa la Yesu Kristo. Ni zipi kati ya hizo ni matokeo ya kazi iliyokamilishwa na Nabii Joseph Smith? Mafundisho na Maagano 135:3 inataja baadhi ya mambo makubwa ambayo Joseph Smith aliyakamilisha katika miaka 24 kufuatia Ono la Kwanza. Ni kwa jinsi gani mambo haya yamekuathiri wewe na mahusiano yako na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Fikiria kuandika ushuhuda wako wa Nabii Joseph Smith. Ni nani angeweza kuhitaji kusikia ushuhuda wako?

Mafundisho na Maagano 136

Bwana ananipa ushauri kwa ajili ya “safari” zangu katika maisha.

Baada ya kufukuzwa kutoka Nauvoo, watakatifu walikabiliwa na safari ndefu kwenda Bonde la Salt Lake, na maili mia moja chache za mwanzo zilikuwa polepole na zenye taabu. Brigham Young, ambaye sasa aliongoza Kanisa kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi ambavyo Watakatifu wangeendelea kuishi mpaka mwisho wa safari ndefu. Aliweka makazi ya muda yaliyoitwa Winter Quarters na aliomba kwa ajili ya mwongozo. Kama jibu, Bwana alimpa ufunuo, sasa sehemu ya 136. Miongoni mwa vitu vingine, ufunuo huu uliwakumbusha Watakatifu “kwamba tabia yao kwenye safari ilikuwa muhimu kama mwisho wa safari” na “ilisaidia kubadili uhamiaji kwenda magharibi kutoka ulazima usio wa muhimu mpaka kwenye uzoefu muhimu wa kiroho wa pamoja” (“Hili Litakuwa Agano Letu,” Ufunuo katika Muktadha 308).

Weka muktadha huu akilini unapojifunza sehemu ya 136. Ni ushauri gani unaoupata ambao ungeweza kusaidia kugeuza jaribu gumu katika maisha yako “kuwa uzoefu muhimu … kiroho”? Unaweza pia kutafakari jinsi ushauri unavyoweza kukusaidia kukamilisha mapenzi ya Bwana katika maisha yako mwenyewe, kama ulivyowasaidia Watakatifu wa mwanzo kufanya safari ndefu kwenda Magharibi.

Ona pia “Hili Litakuwa Agano Letu,” Ufunuo katika Muktadha, 307–14; Church History Topics, “Succession of Church Leadership,” ChurchofJesusChrist.org/study/history/topics.

Picha
Winter Quarters

Winter Quarters, na Greg Olsen

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 135:1, 3.Kuwasaidia wanafamilia kuelewa nini inamaanisha kwamba Joseph Smith “ametia muhuri huduma yake na kazi yake kwa damu yake mwenyewe,” familia yako ingeweza kuangalia video “Testimony of the Book of Mormon” (ChurchofJesusChrist.org; ona pia Jeffrey R. Holland, “Safety for the Soul,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 88–90). Ni nini kinatuvutia kuhusu mistari hii? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa waaminifu zaidi kwenye shuhuda zetu, hata kama hatutakiwi kutoa maisha yetu kwa ajili ya hizo shuhuda?

Mafundisho na Maagano 135:3.Ili kujadili nini inamaanisha kwa kauli kwamba Joseph Smith alifanya “zaidi, isipokuwa Yesu pekee, kwa wokovu wa mwanadamu katika ulimwengu huu, kuliko mwanadamu mwingine yeyote” fikiria kurejea kile familia yako ilichojifunza kuhusu Joseph Smith mwaka huu. Ungeweza kutumia picha kutoka kwenye nyenzo hii kuwasaidia kukumbuka kile walichojifunza na waalike kushiriki hadithi au mafundisho wanayoyapenda. Kwa nini tuna shukrani kwa Nabii Joseph Smith na kwa kile Bwana alichokamilisha kupitia yeye? Ungeweza pia kuangalia video “Joseph Smith: The Prophet of the Restoration” (ChurchofJesusChrist.org).

Mafundisho na Maagano 136.Wakati Bwana alipofunua Sehemu ya 136, Watakatifu walikuwa na safari ndefu, ngumu mbele yao, chini ya maelekezo ya Brigham Young (ona sura ya 5860, na 62 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 206–8, 211–16, 222–24). Mnaposoma sehemu ya 136 pamoja, fikirieni kuhusu vitu vigumu ambavyo familia yenu inaweza kukumbana navyo. Ni ushauri gani tunaupata katika ufunuo huu ambao ungeweza kutusaidia kupata msaada na nguvu za Bwana?

Mafundisho na Maagano 136:4.Ina maana gani “kutembea katika maagizo yote ya Bwana”? Ni kwa jinsi gani maagizo tuliyoyapokea yanaathiri maisha yetu ya kila siku?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Praise to the Man,” Wimbo, na. 27.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Tafuta upendo wa Mungu. Rais M. Russell Ballard alifundisha, “Injili ni injili ya upendo—upendo kwa Mungu na upendo kwetu sisi kwa sisi” (“Upendo wa Mungu kwa Watoto Wake,” Ensign, Mei 1988, 59). Unaposoma maandiko, fikiria kuandika au kuwekea alama ushahidi wa upendo wa Mungu.

Picha
majambazi katika Gereza la Carthage wakimshambulia Joseph Smith na wengine

Hakuna Aliye na Upendo Mwingi, na Casey Childs

Chapisha