Sura ya 58 Kiongozi Mpya kwa ajili ya Kanisa Julai–Agosti 1844 Baada ya Nabii Joseph Smith kuuawa, Kanisa halikuwa na Rais. Watakatifu hawakuwa na uhakika ni nani aliyepaswa kuwa kiongozi wao. Wengi wa Mitume walikuwa mbali kwenye misheni. Sidney Rigdon alikuwa mshauri wa Joseph Smith. Lakini hakuwa amemtii Bwana na alikuwa ameondoka Nauvoo. Mafundisho na Maagano 124:108–109 Wakati Sidney Rigdon aliposikia kwamba Joseph Smith alikuwa amefariki, alirudi Nauvoo. Alitaka kuwa kiongozi wa Kanisa. Mitume waliokuwa mbali katika misheni pia walirudi Nauvoo waliposikia juu ya kifo cha Joseph. Brigham Young alikuwa kiongozi wa Mitume. Alisema Bwana alikuwa amewapa mitume mamlaka ya kuongoza Kanisa hadi Rais mpya atakapochaguliwa. Mafundisho na Maagano 107:24 Waumini wa Kanisa walikuwa na mkutano. Kwanza Sidney Rigdon alizungumza nao na kusema alipaswa kuwa kiongozi wa Kanisa. Kisha Brigham Young alizungumza na kusema Mitume walipaswa kuongoza Kanisa. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. Sauti ya Brigham Young iikuwa kama sauti ya Joseph Smith, na kwa baadhi ya watu alionekana kama Joseph Smith. Watakatifu walijua kwamba Mungu aliwachagua Mitume ili kuongoza Kanisa, na wote walipiga kura ya kuwakubali Mitume kama viongozi wao. Sidney Rigdon alikasirika. Alirudi nyumbani kwake na kuanzisha kanisa lake mwenyewe. Hakuwa tena muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho.