Hadithi za Maandiko
Sura ya 48: Joseph Smith Anamwomba Rais Msaada: Machi–Novemba 1839


Sura ya 48

Joseph Smith Anamwomba Rais Msaada

Machi–Novemba 1839

wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
Joseph akiandika barua

Joseph Smith aliandika barua kwa Watakatifu wakati alipokuwa katika jela ya Liberty. Aliwaambia waandike mambo mabaya ambayo magenge ya watu wenye fujo walikuwa wamewafanyia. Alisema walipaswa kutuma kile walichoandika kwa viongozi wa nchi.

Watakatifu wakiandika majina ya washambuliaji

Joseph aliwaambia Watakatifu kuandika majina ya watu ambao waliwashambulia. Alisema walipaswa kueleza jinsi makazi yao na mashamba yao yalivyoharibiwa.

Joseph na marafiki wakiondoka katika jela ya Liberty

Baada ya Joseph na marafiki zake kuwa katika jela ya Liberty kwa zaidi ya miezi minne, baadhi ya walinzi waliwapeleka mji mwingine kwa ajili ya kesi. Joseph na marafiki zake walinunua farasi wawili kutoka kwa walinzi. Waliwapa walinzi baadhi ya nguo ili kulipia farasi mmoja na kuahidi kulipia farasi mwingine baadaye.

Joseph na marafiki wakitoroka

Usiku mmoja baadhi ya walinzi walilewa na kwenda kulala. Mlinzi mwingine aliwasaidia Joseph na marafiki zake kutoroka.

Joseph na marafiki wakisafiri

Joseph na marafiki zake walifanya zamu kupanda farasi hao. Baada ya siku 10 walifika Quincy, Illinois, ambapo walikuta familia zao.

Joseph na marafiki wakisalimiana na familia zao

Joseph na marafiki zake walikuwa na furaha kuwa pamoja na familia zao tena.

Watakatifu katika Nauvoo

Watakatifu walitaka kupata mahali katika Illinois ili kujenga mji wao wenyewe. Walinunua ardhi loevu na yenye matope karibu na Mto Mississippi. Joseph na Watakatifu walifanya kazi kwa bidii kukausha ardhi ili waweze kujenga nyumba na kupanda bustani. Walianza kujenga mji mzuri, ambao waliuita Nauvoo. Nauvoo humaanisha nzuri.

Joseph anakutana na Rais wa Marekani

Wakati Watakatifu walipokuwa wakianza kujenga Nauvoo, Joseph Smith alikwenda kumwona rais wa Marekani. Joseph alimwambia rais kuhusu magenge ya watu wenye fujo katika Missouri. Alieleza jinsi magenge hayo ya watu wenye fujo yalivyochoma nyumba za Watakatifu, kuwaibia mifugo yao, na kuwalazimisha kuondoka kwenye ardhi yao.

Joseph Anamwomba Rais Msaada

Joseph alisema baadhi ya Watakatifu waliuawa. Wengine walifungwa jela. Alimwonyesha rais kile Watakatifu walichokuwa wameandika kuhusu mambo mabaya yaliyotendwa kwao. Joseph alisema viongozi katika Missouri hawangeweza kuwasaidia Watakatifu. Alimuomba rais awasaidie.

Rais alisema asingeweza kusaidia

Rais alisema alijua Watakatifu walikuwa wameteseka, lakini asingefanya kitu cho chote ili kuwasaidia. Kama angewasaidia Watakatifu, watu katika Missouri wangekasirika.

Joseph akiondoka kwa huzuni

Joseph alihuzunika kwa sababu rais hakuweza kuwasaidia Watakatifu. Alirudi Nauvoo.