Sura ya 35 Watakatifu Wanaondoka Jackson County, Missouri Septemba–Desemba 1833 Kwa sababu genge la watu wenye fujo katika Jackson County lilikuwa likisababisha matatizo mengi, Watakatifu walijaribu kupata msaada kutoka kwa gavana wa Missouri. William Phelps na Orson Hyde walikwenda kuonana na gavana. Walimwambia kuhusu genge hilo na jinsi nyumba zao zilivyokuwa zimeharibiwa. Gavana asingeweza kuwasaidia. Aliwaambia wawaombe majaji msaada. Lakini majaji walikuwa marafiki wa lile genge, na hawangeweza kusaida pia. Genge la watu wenye fujo liliwashambulia Watakatifu kwa siku sita. Walivunja makazi yao, kuwadhuru wanaume, na kuvunja duka na kurusha kila kitu sakafuni. Genge la watu wenye fujo liliwafanya Watakatifu kukimbia makazi yao. Ilikuwa ni majira ya baridi, na watu wengi walikufa kwa sababu hawakuwa na makazi katika hali ya baridi, na mvua. Watakatifu walienda sehemu nyingine za Missouri ili kulikimbia genge hilo la watu wenye fujo. Watakatifu walikuwa na huzuni. Nyumba zao, mashamba, na maduka yaliharibiwa. Wanyama wao walikuwa wameibiwa. Gavana na majaji hawakuweza kuwasaidia. Lakini Watakatifu bado walikuwa na imani katika Mungu. Walijua Kanisa la Yesu Kristo lilikuwa la kweli, na walijua kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa Mungu. Wakati Watakatifu walipokuwa wakiteswa Missouri, Joseph Smith alikuwa Kirtland, Ohio. Yesu alimpa Joseph ufunuo ulioeleza ni kwa nini Watakatifu katika Missouri walikuwa na matatizo. Yesu alisema baadhi ya Watakatifu hawakuwa wametii amri. Hawakuwa na umoja, kama watu wa Sayuni wanavyopaswa kuwa. Baadhi yao walibishana na kuneneana mambo mabaya. Wengine walikuwa na wivu, na wengine hawakushirikiana na wengine vitu vyao. Mafundisho na Maagano 101:2, 6–8 Licha ya matatizo haya, Yesu alisema aliwapenda Watakatifu na Hataweza kuwasahau. Alisema wanapaswa kufarijika kwa sababu wenye moyo safi siku moja watarudi na kujenga Sayuni. Yesu aliwaambia Watakatifu kujiandaa kwa ajili ya wakati Yeye atakapokuja tena. Wakati Atakapokuja, watu watapendana na kuwa na amani. Wale ambao waliteswa kwa kumfuata Yesu watabarikiwa. Shetani hatakuwa na uwezo wa kuwadanganya watu. Hakutakuwa na kifo kama inavyojulikana leo. Kila mtu atakuwa na furaha. Mafundisho na Maagano 101:9, 16–19, 22–36