Hadithi za Maandiko
Watu wa Kuwajua


Watu wa Kuwajua

IbrahimuIbrahimu alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Hadithi ya Ibrahimu ipo katika Agano la Kale na Lulu ya Thamani Kuu.

Bennett, John C.John C. Bennett alikuwa Meya wa Nauvoo. Yeye alimgeuka Joseph Smith.

Kapteni AllenKapteni Allen alikuwa kapteni katika Jeshi la Marekani. Aliwaomba wanaume wa Kanisa kuwa katika Kikosi cha Mormoni.

Copley, LemanLeman Copley alikuwa muumini wa Kanisa katika Kirtland, Ohio, ambaye hakuwapa ardhi yake waumini wengine.

Cowdery, OliverOliver Cowdery alimsaidia Joseph Smith kutafsiri mabamba ya dhahabu. Alifanya kazi nyingi ili kulisaidia Kanisa.

EliaElia alirejesha uwezo maalum wa ukuhani kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu ya Kirtland.

EliyaEliya alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Alirejesha uwezo maalum wa ukuhani kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland .

HenokoHenoko alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Yeye alijenga mji wa Sayuni. Hadithi ya Henoko ipo katika Lulu ya Thamani Kuu.

Gavana BoggsGavana Boggs alikuwa gavana wa Missouri. Yeye hakuweza kuwasaidia Watakatifu na alitoa amri ya kuwaondoa kutoka jimboni au kuwaua.

Harris, MartinMartin Harris alimsaidia Joseph Smith kutafsiri mabamba ya dhahabu. Alipoteza kurasa kadhaa za Kitabu cha Mormoni.

Hyde, OrsonOrson Hyde alikuwa Mtume. Aliweka wakfu Nchi Takatifu kwa ajili ya watoto wa Ibrahimu wapate mahali pa kuishi.

WahindiWahindi waliishi katika maeneo yote ya Marekani. Wakati mwingine Wahindi wanaitwa Walamani.

YakoboYakobo alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu. Petro, Yakobo na Yohana, walirejesha Ukuhani wa Melkizedeki kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery.

YohanaYohana alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na wawili wa Yesu. Petro, Yakobo na Yohana, walirejesha Ukuhani wa Melkizedeki kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery.

Yohana MbatizajiYohana Mbatizaji aliishi wakati Yesu alipoishi duniani. Yohana Mbatizaji alitoa Ukuhani wa Haruni kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery.

Kimball, Heber C.Heber C. Kimball alikuwa Mtume. Alikwenda misheni huko Uingereza.

Kimball, SarahSarah Kimball alikuwa mshiriki wa Muungano wa kwanza wa Usaidizi wa Akina Mama.

Kimball, Spencer W.Spencer W. Kimball alikuwa Rais wa 12 wa Kanisa.

Knight, NewelNewel Knight alikuwa mgonjwa wakati Shetani alipojaribu kumzuia kuomba. Joseph Smith alimponya Newel Knight.

WalamaniWalamani ni uzao wa wana wa Lehi, ambao ni Lamani na Lemueli.

MelkizedekiMelkizedeki alikuwa nabii aliyeishi hapo kale.

WamormoniWakati mwingine waumini wa Kanisa wanaitwa Wamormoni kwa sababu wanaamini katika Kitabu cha Mormoni.

MoroniMoroni alikuwa Nabii Mnefi aliyeishi Marekani hapo kale. Alizika mabamba ya dhahabu katika Kilima Kumora.

MusaMusa alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri. Alirejesha uwezo maalum wa ukuhani kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland.

Bw. ChandlerBw. Chandler aliuza baadhi ya magombo ya karatasi za kale kwa Watakatifu huko Kirtland. Maandiko ya Ibrahimu yalikuwa kwenye magombo ya karatasi.

Bw. HaleBw. Hale alikuwa baba yake Emma Smith.

NuhuNuhu alikuwa nabii aliyeishi miaka mingi iliyopita.

Page, HiramHiram Page alisema alikuwa na jiwe lililompa mafunuo kwa ajili ya Kanisa.

Partridge, EdwardEdward Partridge alikuwa askofu wa kwanza wa Kanisa.

PetroPetro alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa Yesu. Petro, Yakobo na Yohana, walirejesha Ukuhani wa Melkizedeki kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery.

Phelps, William W.William W. Phelps alisaidia kuanzisha shule katika Jackson County, Missouri.

WaanzilishiWaanzilishi walikuwa Watakatifu waliovuka uwanda kwenda katika Milima ya Miamba.

Pratt, Parley P.Parley P. Pratt alienda misheni kuwafundisha Walamani.

Richards, WillardWillard Richards alikuwa rafiki wa Joseph Smith. Alikuwa pamoja na Joseph katika Jela ya Carthage.

Rigdon, SidneySidney Rigdon alikuwa mmoja wa washauri wa Joseph.

Smith, AlvinAlvin Smith alikuwa mmoja wa kaka wakubwa wa Joseph Smith. Yeye alifariki. Joseph aliona ono la Alvin akiwa katika ufalme wa selestia wa mbinguni.

Smith, EmmaEmma Smith alikuwa mke wa Joseph Smith. Alikuwa kiongozi wa kwanza wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Alitengeneza kitabu cha nyimbo za dini kwa ajili ya Kanisa.

Smith, HyrumHyrum Smith alikuwa mmoja wa kaka mkubwa wa Joseph Smith. Hyrum aliuawa katika Jela ya Carthage pamoja na Joseph.

Smith, JosephJoseph Smith alikuwa nabii wa kwanza na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Yesu alimpa Joseph Smith mafunuo ambayo yanapatikana katika Mafundisho na Maagano. Joseph aliuawa katika Jela ya Carthage.

Smith, Joseph Sr.Joseph Smith Mkubwa alikuwa baba yake Joseph Smith.

Smith, LucyLucy Smith alikuwa mama yake Joseph Smith.

Smith, SamuelSamuel Smith alikuwa kaka mdogo wa Joseph Smith. Alikuwa mmisionari wa kwanza wa Kanisa.

Snow, Eliza R.Eliza R. Snow alikuwa mshiriki wa Muungano wa wa kwanza wa Usaidizi wa Akina Mama.

Taylor, JohnJohn Taylor alikuwa rafiki wa Joseph Smith. Alikuwa pamoja na Joseph katika Jela ya Carthage. Baadaye alikuwa Rais wa Kanisa.

Whitmer, DavidDavid Whitmer alikuwa shahidi aliyeona mabamba ya dhahabu. Alisaidia kuanzisha Kanisa mnamo 6 Aprili 1830.

Whitmer, PeterPeter Whitmer alisaidia kuanzisha Kanisa mnamo 6 Aprili 1830.

Whitney, Newel K.Newel K. Whitney alikuwa askofu wa pili wa Kanisa.

Williams, Frederick G.Frederick G. Williams alikuwa mmoja wa washauri wa Joseph Smith.

Young, BrighamBrigham Young alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili. Alikuwa kiongozi wa waanzilishi. Alikuwa Rais wa Kanisa baada ya Joseph Smith.

Young, PhineasPhineas Young alikuwa kaka wa Brigham Young.