Scripture Stories
Sura ya 5: Joseph Smith na Oliver Cowdery: Februari–Aprili 1829


Sura ya 5

Joseph Smith na Oliver Cowdery

Februari–Aprili 1829

Picha
mabamba ya dhahabu
Picha
Joseph Smith Mkubwa anamtembelea Joseph

Joseph na Emma Smith waliishi katika shamba dogo karibu na Harmony, Pennsylvania. Baba yake Joseph alikuja kuwatembelea. Walikuwa na furaha kumwona. Baba yake Joseph alikuwa mtu mwema.

Picha
Joseph anapokea ufunuo

Yesu alimpa Joseph ufunuo kwa ajili ya baba yake. Ufunuo ulieleza jinsi ambavyo watu wangeweza kumsaidia Yesu. Wanapaswa kumpenda Yesu. Wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kufundisha injili. Wanapaswa kuwapenda na kuwasaidia watu wengine.

Picha
Joseph Smith Mkubwa akiomba

Watu waonataka kumsaidia Yesu wanapaswa pia kuomba na kuwa na imani. Yesu alisema watu wanaomsadia watabarikiwa.

Picha
Joseph Smith Mkubwa akiondoka kwa Joseph na Emma

Baba yake Joseph alikwenda nyumbani na kujaribu kufanya mambo ambayo Yesu alimwambia kufanya. Alishiriki injili na wengi wa wana familia yake.

Picha
Joseph akiomba

Ilimbidi Joseph afanye kazi katika shamba lake. Pia alihitaji kutafsiri mabamba ya dhahabu. Ilikuwa kazi kubwa mno kwake kufanya peke yake, hivyo alisali na kumwomba Baba wa Mbinguni kwa ajili ya usaidizi.

Picha
Joseph anakutana na Oliver Cowdery

Baba wa Mbinguni alijibu maombi ya Joseph. Alimtuma mtu mmoja aliyeitwa Oliver Cowdery kwa Joseph. Oliver alitaka kujua kuhusu mabamba ya dhahabu. Joseph alimwambia kuhusu malaika Moroni, mabamba, na Kitabu cha Mormoni.

Picha
Oliver Cowdery akinakili

Oliver alimwamini Joseph na kusema angesaidia kutafsiri mabamba ya dhahabu. Wakati Joseph akisoma maneno kwa sauti, Oliver aliyaandika kwenye karatasi. Joseph na Oliver walifanya kazi kwa bidii.

Picha
Joseph na Oliver

Yesu aliwafundisha Joseph na Oliver mambo mengi. Alisema wanapaswa kutafuta hekima na uzima wa milele, si utajiri. Alisema pia wanapaswa kujifunza juu ya Mungu na kuwasaidia watu kujifunza injili. Wanapaswa kuwa waaminifu na kufanya mambo mema. Ikiwa wangefanya hivyo, wangeweza kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni milele.

Picha
Oliver akiwa tayari kutafsiri

Yesu alisema Oliver anapaswa daima kuwa rafiki wa Joseph na kumsaidia katika nyakati ngumu. Yesu pia alisema Oliver angeweza kujifunza kutafsiri kama Joseph. Roho Mtakatifu angemsaidia Oliver kutafsiri ikiwa Oliver alikuwa na imani ya kutosha.

Picha
Oliver akijaribu kutafsiri

Oliver alijaribu kutafsiri. Alidhani ingekuwa rahisi, lakini hakuweza.

Picha
Joseph akiomba

Yesu alisema Oliver hakuwa ameomba msaada wa Mungu katika njia sahihi. Yesu alimwambia Joseph Smith jinsi Oliver na watu wote wanavyoweza kupata msaada kutoka kwa Mungu.

Picha
msichana akisoma maandiko

Wakati watu wanapohitaji msaada, wanapaswa kufikiri kwa makini kuhusu nini cha kufanya. Wanapaswa kuamua kile wanachofikiri ni jambo sahihi kufanya.

Picha
msichana akiomba

Kisha wanapaswa kumwuliza Mungu ikiwa ni sahihi. Kama ni sahihi, watajisikia vizuri katika mioyo yao. Watajua ni sahihi.

Picha
msichana akiomba

Kama si sahihi, hawatajisikia vizuri katika mioyo yao.

Picha
Joseph akisoma mabamba

Oliver hakujaribu kutafsiri Kitabu cha Mormoni tena. Badala yake, aliandika maneno wakati Joseph akiyatafsiri. Yesu alisema Oliver angebarikiwa kwa kumsaidia Joseph.

Chapisha