Scripture Stories
Sura ya 25: Joseph Smith na Sidney Rigdon Wanaenda Misheni: Desemba 1831–Januari 1832


Sura ya 25

Joseph Smith na Sidney Rigdon Wanaenda Misheni

Desemba 1831–Januari 1832

Picha
gari la kukokotwa na maksai
Picha
waumini wakionyesha kwenye gazeti

Baadhi ya watu walikuwa wakichapisha uongo juu ya Kanisa kwenye gazeti. Yesu aliwaambia Joseph Smith na Sidney Rigdon waende misheni kwenye miji mingine na kuwaambia watu ukweli kuhusu Kanisa.

Picha
Joseph na Sidney wakisafiri wakati wa baridi

Joseph na Sidney walimtii Yesu. Waliacha nyumba zao na kwenda katika miji mingi. Walizungumza katika mikutano ya kanisa na kuwafundisha watu katika makazi yao.

Picha
Sidney Rigdon

Joseph na Sidney waliwaambia watu kuhusu amri za Mungu. Walishuhudia kuhusu Yesu Kristo na waliwaambia watu watubu. Wakati Joseph na Sidney walipomaliza misheni zao, walirudi nyumbani kwa familia zao.

Chapisha