Hadithi za Maandiko
Sura ya 41: Matatizo katika Kirtland: 1837–1838


Sura ya 41

Matatizo katika Kirtland

1837–1838

wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
familia

Watakatifu katika Kirtland, Ohio, walikuwa na furaha. Bwana aliwabariki.

mzee akifundisha injili

Baadhi ya wazee waliondoka Kirtland na kwenda kufundisha injili katika maeneo mengine. Watu wengi waliwasikiliza wazee na kujiunga na Kanisa.

watu wakiwa benki huko Kirtland.

Kisha matatizo yalianza Kirtland. Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa walianzisha benki ambapo Watakatifu wengi walitunza fedha zao.

mtu akiiba fedha kutoka benki

Baadhi ya Watakatifu walitaka kupata fedha nyingi. Mtu mmoja aliyefanya kazi benki hakuwa mwaminifu. Aliiba baadhi ya fedha.

wanaume wakiwa na huzuni

Joseph Smith aliwaambia watu wengine kutunza fedha vizuri, lakini benki iliendelea kuwa na matatizo. Punde ilibidi ifungwe kwa sababu fedha zote zilitoweka. Huu ulikuwa wakati mgumu kwa benki nyingi nchini Marekani, na nyingine nyingi zilifungwa.

Watakatifu wenye hasira

Wengi wa Watakatifu walikuwa na hasira kwa sababu hawakuweza kupata fedha zao. Baadhi yao walisema lilikuwa kosa la Joseph Smith kwamba benki ilifungwa. Baadhi ya marafiki wakubwa wa Joseph walisema mambo mabaya juu yake. Baadhi ya watu hata walitaka kumuua.

viongozi wakiondoka Kanisani

Baadhi ya viongozi wa Kanisa walikuwa na hasira pia. Baadhi yao hawakutaka tena kuwa waumini wa Kanisa. Wachache wao wakawa maadui wa Kanisa.

Brigham Young akizungumza na watu

Viongozi wengine wa kanisa walimpenda Joseph na walimsaidia. Brigham Young alikuwa mmoja wa viongozi wema. Aliwaambia Watakatifu kwamba yeye alijua Joseph alikuwa nabii wa Mungu. Baadhi ya watu walimkasirikia Brigham Young kwa kumuunga mkono Nabii, na ilimbidi kuondoka Kirtland ili wasiweze kumdhuru.

genge la watu wenye fujo likiwashambulia watu Kirtland

Maadui wa Kanisa walizua matatizo mengi Kirtland. Waliiba vitu kutoka kwa Watakatifu na kuharibu nyumba zao. Pia waliwadhuru Watakatifu na kutishia kuwaua baadhi yao.

genge la watu wenye fujo likibishana kuhusu Joseph

Baadhi ya wazee wa Kanisa walifanya mikutano katika Hekalu la Kirtland ambapo walimkosoa Joseph Smith na kuzungumza kuhusu kumweka kiongozi mpya katika nafasi yake. Baadaye baadhi ya watu walitumia bunduki na visu ili kujaribu kulitwaa hekalu. Punde ikawa si salama kwa Joseph kukaa Kirtland, hivyo aliondoka mnamo Januari 1838 na kwenda Missouri.

waumini wakiondoka Kirtland

Kwa sababu ya mateso mengi katika Kirtland, viongozi wa Kanisa walianza kufanya mipango ili Watakatifu waondoke. Mnamo Julai 1838, zaidi ya waumini 500 wa Kanisa waliondoka Kirtland. Mnamo Oktoba, baada ya safari ngumu ya karibu maili 1,000, walifika Far West, Missouri. Joseph Smith na waumini wengine wengi wa Kanisa walikuwa wakiishi huko.