Sura ya 30 Ufunuo kuhusu Vita Desemba 25, 1832 Watu wengi walikuwa wakibatizwa katika Kanisa. Injili iliwafanya wawe na furaha, lakini walikuwa na wasiwasi kuhusu mambo yaliyokuwa yanatokea duniani. Matetemeko ya ardhi na vita vilikuwa vikitokea katika sehemu nyingi. Mambo ya kusikitisha pia yalikuwa yakitokea Marekani. Baadhi ya watu hawakutaka kuwa sehemu ya nchi. Walitaka kuwa na viongozi wao wenyewe. Mnamo Siku ya Krismasi 1832, Yesu alimpa Joseph Smith ufunuo kuhusu vita. Mafundisho na Maagano 87 Yesu alisema watu nchini Marekani wangepigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Unabii huu ulitimizwa wakati Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe ya Marekani ilipoanza miaka 30 baadaye. Mafundisho na maagano 87:1–3 Yesu pia alifunua kwamba kutakuwa na vita katika maeneo mengine yote ya dunia. Watu wengi watakufa, na kutakuwa na huzuni ya kutisha. Yesu alisema Watakatifu wanapaswa kuwa waaminifu katika nyakati hizi ngumu. Mafundisho na maagano 87:3–8 Joseph Smith alisikitika kujua kwamba kutakuwa na vita vingi hivyo. Alijua kwamba kama watu watatii amri za Mungu, wasingeweza kupigana na kuwa na vita.