Hadithi za Maandiko
Sura ya 17: Maaskofu wa Kwanza wa Kanisa: Februari na Desemba 1831


Sura ya 17

Maaskofu wa Kwanza wa Kanisa

Februari na Desemba 1831

ubatizo
Joseph akifungasha

Baadhi ya watu katika New York walikuwa wakatili kwa Watakatifu na waliwataka waondoke. Yesu alimwambia Joseph Smith kuondoka New York na kwenda Kirtland, Ohio.

Joseph akielekea Kirtland

Joseph na Emma, Sidney Rigdon, na Edward Partridge walikwenda Kirtland. Joseph na Emma waliishi na muumini wa Kanisa aliyeitwa Newel K. Whitney.

waumini wa Kanisa

Kulikuwa na karibu waumini 1,000 wa Kanisa katika Kirtland. Walikuwa wakijaribu kumtii Mungu, lakini hawakuelewa injili yote.

Mafundisho na Maagano 41, kichwa cha habari cha sehemu

Edward Partridge

Joseph aliomba na kupokea ufunuo. Yesu alimwambia kwamba Watakatifu katika Kirtland walimhitaji askofu. Askofu angepaswa kutumia muda wake kufundisha na kuwasaidia Watakatifu. Askofu wa kwanza katika Kanisa alipaswa kuwa Edward Partridge.

Newell K. Whitney

Kadiri watu wengi walivyojiunga na Kanisa, maaskofu zaidi walihitajika. Newel K.Whitney aliitwa kuwa askofu wa pili wa Kanisa.

Watakatifu kwenye ghala la askofu

Yesu alimwambia Joseph kwamba askofu angepaswa kusimamia ghala. Watakatifu wangepaswa kutoa chakula, mavazi, na matoleo mengine kwa askofu ili kuweka katika ghala hilo. Kisha askofu angetumia vitu hivi ili kuwasaidia Watakatifu ambao ni masikini au wenye shida.

mtu akihesabu pesa

Yesu pia alisema kwamba askofu anapaswa kupokea fedha ambazo Watakatifu wanazitoa kwa Kanisa. Askofu angetumia fedha hizi ili kulipia matumizi ya Kanisa na kusaidia masikini.

askofu anakutana na waumini wake

Askofu anapaswa kuwapenda Watakatifu na kujaribu kuwasaidia. Anapaswa kukutana na wanaume wenye ukuhani na kujadiliana nao juu ya kile wanachokifanya ili kuwasaidia Watakatifu.

askofu akiwahubiria waumini wake

Askofu huongoza Watakatifu katika kila kata. Rais wa tawi ni kama askofu. Rais wa tawi huongoza Watakatifu katika kila tawi.

maaskofu katika Kanisa

Leo kuna maelfu ya maaskofu katika Kanisa.