Hadithi za Maandiko
Sura ya 19: Ujio wa Pili wa Yesu Kristo


Sura ya 19

Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

ubatizo
watu wanawapigia kelele Watakatifu

Baadhi ya watu huko Kirtland, Ohio, hawakutaka kujifunza injili. Baadhi hata walisema uongo kuhusu Watakatifu ili kujaribu kuwazuia wengine kujifunza kuhusu injili.

Mafundisho na Maagano 45, kichwa cha habari cha sehemu

Joseph akishiriki Kitabu cha Mormoni

Yesu alimwambia Joseph Smith kuwa Yeye angerudi duniani tena hivi karibuni. Kabla ya Yeye kuja, kila mtu duniani lazima aisikie Injili. Watakatifu wanapaswa kuwa wamisionari wema na kufanya kazi kwa bidii ili kushiriki injili.

Yesu akiwafundisha Mitume wake

Wakati Yesu alipoishi duniani, Aliwaambia Mitume Wake kile kitakachotokea kabla ya Yeye kurudi tena.

ishara za siku za mwisho

Yesu aliwaambia Mitume Wake kwamba hekalu la Yerusalemu lingeharibiwa. Wayahudi watatawanyika kwenye mataifa mengi, na wengi wao watauawa. Kutakuwa na vita nyingi. Watu hawatapendana, na watageuza mioyo yao kutoka kwa Mungu. Kutakuwa na magonjwa ya kutisha, maradhi, na matetemeko ya ardhi. Jua litakuwa giza, mwezi utakuwa kama damu, na nyota zitaanguka.

Ono la Kwanza la Joseph Smith

Tukio moja muhimu katika maandalizi kwa ajili ya kurudi kwa Yesu duniani ni urejesho wa Kanisa Lake. Yesu alisema injili iliyorejeshwa itakuwa kama nuru katika giza.

askari wakipigana vitani

Mambo mengi ambayo Yesu alizungumza kuyahusu tayari yametokea. Mambo mengine yanaanza kutokea, na mengine yatatokea katika siku zijazo.

Wayahudi wakirudi Yerusalemu

Wakati mambo haya yatakapotokea, watu wenye haki watajua Yesu anakuja karibuni. Watamtaka Yeye aje. Wayahudi wengi watarudi Yerusalemu. Wataisikia injili.

Watakatifu wakijenga Sayuni Mpya

Watakatifu wenye haki watajenga mji mpya wa Sayuni, ambapo watakuwa salama. Hawatapigana wao kwa wao. Watakuwa na furaha na kuimba nyimbo za shangwe. Watu ambao si wenye haki hawataweza kwenda Sayuni.

Yesu akitokea mawinguni

Yesu atakuja duniani katika wingu angavu. Watu wenye haki watamwona. Watu wote wenye haki waliokufa watafufuliwa. Watakutana na Yesu mawinguni na kuja duniani pamoja Naye.

Yesu anakuja Yerusalemu

Yesu atakuja Yerusalemu. Atasimama juu ya mlima pale, na utagawanyika mara mbili. Mbingu na nchi zitatikisika. Watu waovu wataangamizwa.

Wayahudi wakilia kwenye majeraha ya Yesu

Watu katika Yerusalemu watamwona Yesu na kuuliza, “Je, haya majeraha katika mikono na miguu yako ni ya nini?” Atasema: “Mimi ni Yesu ambaye alisulubiwa. Mimi ni Mwana wa Mungu.” Ndipo watu watakapolia kwa sababu ya uovu wao na kuomboleza kwa sababu Yesu alikuwa ameteswa.

Yesu anaishi na Watakatifu

Watu wenye haki watakuwa na furaha tele kumwona Yesu. Dunia nzima itakuwa ni mali yao. Shetani hataweza kuwajaribu. Watoto wao watakua bila dhambi. Yesu ataishi pamoja nao kwa miaka 1,000 na atakuwa Mfalme wao.

wamisionari wakifundisha familia

Yesu alimwambia Joseph Smith kuwatuma wamisionari ili wawaambie watu kutubu na kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili. Yesu alisema Watakatifu pia wanapaswa kujiandaa. Wanapaswa kuomba, kufunga, na kufundishana amri.

familia imepiga magoti katika kuomba

Yesu aliwaahidi Watakatifu kwamba kama wangekuwa karibu Naye, Angekuwa karibu nao. Alisema wanapaswa kuomba, na Yeye aliahidi kwamba Mungu angewajibu.

familia ikishiriki chakula

Watakatifu wanapaswa kufanya kila kitu wanachoweza ili kumsaidia Yesu. Wakati watu wanapomsaidia Yesu, wanakuwa kama Yeye. Ndipo watakuwa tayari kwa Ujio Wake wa Pili.