Scripture Stories
Sura ya 51: Endaumenti za Kwanza: Mei 1842


Sura ya 51

Endaumenti za Kwanza

Mei 1842

Picha
Hekalu la Nauvoo
Picha
Hekalu la Nauvoo

Yesu alimwahidi Joseph Smith kwamba Angewapa Watakatifu baraka maalum. Baraka hii inaitwa endaumenti. Endaumenti inatolewa hekaluni. Ni wanaume na wanawake ambao wanatii amri za Mungu ndio pekee wanaoweza kupokea endaumenti.

Picha
Joseph akifundisha kuhusu hekalu

Baadaye, Joseph Smith alifanya mkutano na baadhi ya wanaume na wake zao. Aliwafundisha mambo ambayo wangeweza kufanya hekaluni. Kisha endaumenti zilitolewa kwao wote.

Picha
hekalu la siku za leo

Waumini wa Kanisa ambao wanatii amri za Mungu wanaweza kwenda hekaluni na kupokea baraka maalum ya endaumenti. Kama sehemu ya endaumenti, wanafanya maagano na Mungu, na Yeye anafanya maagano pamoja nao.

Chapisha