Scripture Stories
Sura ya 64: Watakatifu katika Milima ya Miamba: Kuanzia Julai 1847


Sura ya 64

Watakatifu katika Milima ya Miamba

Kuanzia Julai 1847

Picha
kuelekea magharibi
Picha
Brigham Young akionyesha

Waanzilishi walianza kujenga mji katika Bonde Kuu la Salt Lake. Waliuita Mji wa Salt Lake. Brigham Young alichagua mahali pa kujenga hekalu.

Picha
wanaume wakipanda na kujenga

Brigham Young na viongozi wengine waliweka mipango kwa ajili ya mji. Kila familia ilipewa sehemu ya ardhi kwa ajili ya nyumba na shamba. Waanzilishi walijenga nyumba za magogo na kupanda mazao. Walijua ingehitaji imani kubwa na kazi ngumu kuweza kuishi hapa, lakini waliamini wangefanikiwa kwa msaada wa Mungu.

Picha
wanaume wakiweka viunzi vya kanisa jipya

Brigham Young aliugawa mji katika kata tano, na watu walianza kujenga makanisa. Kadiri waanzilishi zaidi walivyovuka tambarare na kuelekea kwenye bonde, kata zaidi ziliundwa.

Picha
mwanamke akiwafundisha watoto

Waanzilishi walianzisha shule. Madarasa ya shule na mikutano ya Kanisa vilifanyika katika jengo moja. Baadaye Shule ya Jumapili ilianzishwa.

Picha
wamisionari wakimfundisha mtu

Brigham Young aliwatuma wamisionari kwenye nchi zingine ng’ambo ya bahari. Maelfu ya watu kutoka nchi nyingi walijiunga na Kanisa.

Picha
waumini wapya wakisafiri kwa meli

Watu wengi ambao walijiunga na Kanisa walihimizwa kukusanyika na Watakatifu katika Bonde Kuu la Salt Lake. Walitoa dhabihu kuu kuacha nyumba zao, kusafiri melini kuvuka bahari, na kusafiri kuvuka Marekani hadi Bonde la Salt Lake.

Picha
waanzilishi wakisafiri

Wengi wa waanzilishi walivuka tambarare katika magari ya kukokotwa na maksai yaliyofunikwa, ambayo yalivutwa na wanyama. Wengine hawakuwa na fedha za kununua magari ya kukokotwa na maksai au wanyama, hivyo walitengeneza mikokoteni midogo yenye magurudumu mawili. Hii iliitwa mikokoteni ya mkono. Waanzilishi waliweka vitu vyao vyote katika mikokoteni, kisha walisukuma na kuvuta mikokoteni kuvuka tambarare. Ilikuwa kazi ngumu sana kuvuka tambarare. Baadhi ya watu waliugua na kufa.

Picha
Watakatifu wakiendesha gari la kukokotwa na maksai lililofunikwa

Brigham Young alikuwa kiongozi mwenye busara. Aliwatuma Watakatifu kujenga miji katika sehemu nyingi za magharibi, ikiwa ni pamoja na Idaho, Wyoming, Arizona, na California.

Picha
watakatifu shambani

Watakatifu walikuwa na majaribu mengi. Wakati mwingine mazao yao hayakukua kwa sababu kulikuwa na baridi kali au joto kali na ukavu. Wakati mwingine wadudu walikula mazao yao. Lakini Watakatifu waliomba na walikuwa na imani, na Mungu aliwasaidia kupitia majaribu yao.

Picha
Wenyeji wa Amerika wakishiriki chakula

Baadhi ya Wahindi walikuwa wakiishi katika eneo hilo wakati Watakatifu walipowasili. Wakati mwingine kulikuwa na matatizo kati ya Watakatifu na Wahindi. Brigham Young aliwaambia Watakatifu wawe wakarimu. Wengi wa Wahindi walikuwa marafiki zao, na baadhi yao walikuwa waumini wa Kanisa.

Picha
mwanamume akifanya kazi katika Hekalu la Salt Lake

Watakatifu walianza kujenga mahekalu, kama vile walivyofanya huko Kirtland na Nauvoo. Mnamo 1853 walianza kujenga hekalu katika Mji wa Salt Lake. Walifanya kazi miaka 40 ili kulikamilisha. Walijenga mahekalu mengine katika miji ya St. George, Logan, na Manti kabla ya Hekalu la Salt Lake kukamilika.

Chapisha