Scripture Stories
Sura ya 59: Endaumenti Zinafanyika katika Hekalu la Nauvoo: Novemba 1845–Februari 1846


Sura ya 59

Endaumenti Zinafanyika katika Hekalu la Nauvoo

Novemba 1845–Februari 1846

Picha
Hekalu la Nauvoo
Picha
Watakatifu wakifanya kazi kwenye hekalu la Nauvoo

Baada ya kifo cha Joseph Smith, Watakatifu waliendelea kufanyia kazi Hekalu la Nauvoo. Bwana alikuwa amewaambia wajenge hekalu, na walitaka kumtii. Watakatifu walifanya sehemu kubwa ya kazi hii wakati walipokuwa wakiteswa na walijua punde ingewabidi waondoke Nauvoo.

Picha
Watakatifu wakikamilisha hekalu

Wakati kila sehemu ya hekalu ilipokamilika, Watakatifu waliiweka wakfu na kuanza kuitumia. Ubatizo kwa ajili ya wafu ulikuwa umefanywa hekaluni tangu 1841, wakati sehemu ya chini ilpokamilika. Mnamo Novemba 1845, vyumba kadhaa vya ghorofani vilikamilika na kuwekwa wakfu kwa ajili ya Watakatifu kupokea ibada takatifu ya endaumenti (ona pia sura ya 50).

Picha
Hekalu la Nauvoo

Watakatifu walikuwa na hamu kubwa ya kupokea ibada zao za hekaluni kiasi kwamba walitumia hekalu usiku na mchana. Wakati wa wiki chache za mwisho kabla ya Watakatifu kuondoka Nauvoo, Brigham Young na wengine walitoa muda wao wote kuwasaidia kupokea ibada hizi. Kufikia wakati ambapo Watakatifu waliondoka, karibu 6,000 kati yao walikuwa wamepokea endaumenti zao katika Hekalu la Nauvoo. Ibada hizi zilikuwa baraka kuu kwao pale walipokuwa wakivumilia majaribu magumu ya miaka iliyofuatia.

Chapisha