Hadithi za Maandiko
Sura ya 49: Wamisionari katika Nchi Zingine: Juni 1837–Oktoba 1841


Sura ya 49

Wamisionari katika Nchi Zingine

Juni 1837–Oktoba 1841

wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
meli kubwa baharini

Bwana alitaka watu katika nchi zingine kujifunza juu ya injili. Mnamo 1837, wakati Watakatifu wengi walipokuwa Kirtland, Bwana alimwambia Joseph Smith kwamba Mzee Heber C. Kimball alitakiwa kwenda misheni huko Uingereza. Mzee Kimball alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili, na yeye pamoja na wamisionari wengine sita walisafiri hadi Uingereza kwa meli.

wamisionari wakihubiri

Wamisionari walikutana na kiongozi wa kanisa jingine ambaye aliwaruhusu kuhubiri katika kanisa lake. Watu wengi waliwaamini wamisionari na walitaka kubatizwa. Kiongozi alikuwa na hasira na kusema wamisionari hawangeweza kuhubiri katika kanisa lake tena.

wamisionari wakihubiri

Wamisionari walihubiri katika makazi ya watu. Watu wengi walijiunga na Kanisa.

Joseph akizungumza na wamisionari

Mnamo1839, baada ya Watakatifu kuanza kujenga Nauvoo, Mitume Kumi na Wawili waliitwa kwenda Uingereza ili kuendelea kuhubiri Injili huko. Kabla ya kusafiri, Joseph Smith alikutana nao na kuwaambia kile walichopaswa kufundisha.

Joseph akizungumza na wamisionari

Joseph aliwaambia wamisionari watii amri za Mungu. Alizungumza nao juu ya ukuhani. Alisema kwamba Kanisa la kweli la Yesu Kristo ndilo pekee lenye ukuhani.

wamisionari wakiziacha familia zao

Wanaume walikuwa tayari kwenda kwenye misheni zao. Ilikuwa ni vigumu kuondoka kwa sababu hawakuwa na fedha nyingi, wengi wao walikuwa wagonjwa, na baadhi ya wake zao na watoto wao walikuwa wagonjwa. Lakini wanaume walikuwa na imani kwamba Baba wa Mbinguni angewasaidia na angebariki familia zao.

mmisionari akimbatiza mwanamke

Wamisionari walienda Uingereza na kuhubiri katika miji mingi. Maelfu ya watu waliamini injili na kujiunga na Kanisa. Wengi wa wale ambao walibatizwa walienda Marekani na walikuwa nguvu kubwa kwa Kanisa.

Orson Hyde akibariki Nchi Takatifu

Orson Hyde alikuwa mmoja wa Mitume. Joseph Smith alisema Orson alikuwa na kazi maalum ya kufanya kwa Wayahudi. Baada ya miezi kadhaa huko Ulaya, Mzee Hyde alienda katika Nchi Takatifu, ambayo ni mahali Yesu alipoishi wakati alipokuwa duniani. Mnamo Oktoba 24 1841, Mzee Hyde alitoa sala ya kuweka wakfu Nchi Takatifu.

Nchi Takatifu

Katika sala yake, Mzee Hyde aliomba Mungu kubariki nchi kwa ajili ya mkusanyiko wa Wayahudi. Alisema kwamba Mungu alikuwa ametoa nchi hii kwa Ibrahimu na watoto wake, kwamba watoto hawa walikuwa wametawanyika, na kwamba walitazamia kutimizwa kwa ahadi za Mungu. Mzee Hyde pia alibariki nchi ili iweze kuwa na maji ili chakula kiweze kukua.

Rais Spencer W. Kimball katika Nchi Takatifu

Miaka mingi tangu sala ya Mzee Hyde, Wayahudi wengi na watoto wengine wa Ibrahimu wamekusanyika katika Nchi Takatifu. Mnamo 1979, Rais Spencer W. Kimball alitoa sala ya kuweka wakfu bustani huko. Inaitwa Bustani ya makumbusho ya Orson Hyde.