Sura ya 37
Viongozi wa Ukuhani
Februari–Machi 1835
Joseph Smith aliwaomba wanaume wa Kambi ya Sayuni pamoja na wengine kuja kwenye mkutano muhimu katika Kirtland, Ohio. Joseph aliwaambia wanaume kwamba Yesu alitaka mitume kumi na wawili waitwe ili kusaidia kuongoza Kanisa.
Bwana alikuwa amemwambia Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris kuchagua Mitume. Kwenye mkutano, Oliver, David, na Martin walibarikiwa na Urais wa Kwanza wa Kanisa. Kisha wakaomba pamoja na kuchagua wanaume wema kumi na wawili.
Wanaume kumi na wawili walitawazwa kuwa Mitume. Kuitwa kwa Mitume ilikuwa ni moja ya matukio muhimu zaidi katika urejesho wa Kanisa la Bwana.
Mitume ni viongozi muhimu sana katika Kanisa. Wanajua kwamba Yesu ni Mwokozi wetu. Wanafundisha injili ulimwenguni kote.
Baada ya siku chache, wanaume wengine walichaguliwa kuwa viongozi katika Kanisa. Waliitwa Sabini. Sabini waliwasaidia Mitume.
Siku moja Mitume Kumi na Wawili walikuwa katika mkutano. Walikuwa wakijitayarisha kwenda misheni, na walitaka usaidizi wa Baba wa Mbinguni.
Mitume walimwomba Joseph Smith kuomba kwa ajili ya ufunuo ili kuwasaidia katika misheni zao. Yesu alimpa Joseph na Mitume ufunuo mkuu ambao ndani yake aliwaambia kuhusu ukuhani.
Mafundisho na Maagano 107, kichwa cha habari cha sehemu
Ukuhani ni uwezo wa Mungu. Ni uwezo mkuu zaidi duniani. Mungu anatoa ukuhani kwa watu waadilifu. Wanaume ambao wana ukuhani wanaweza kuruhusiwa kuhubiri injili, kufanya ibada, na kuwa viongozi katika Kanisa.
Kuna ukuhani wa aina mbili katika Kanisa. Moja ni ukuhani wa Melkizedeki, ambao pia huitwa ukuhani mkuu zaidi. Rais wa Kanisa, washauri wake, Mitume Kumi na Wawili, na Sabini wote wana Ukuhani wa Melkizedeki.
Rais wa Kanisa ni Nabii wa Mungu. Yeye anawaambia watu yale ambayo Yesu anataka wafanye. Nabii ana washauri ambao humsaidia. Nabii na washauri wake ni Urais wa Kwanza wa Kanisa.
Makuhani wakuu pia wana Ukuhani wa Melkizedeki. Viongozi wengi katika vigingi na kata ni makuhani wakuu. Hawa ni pamoja na marais wa vigingi, Maaskofu, na wajumbe wa baraza kuu.
Wanaume ambao wametawazwa kama wazee pia wana Ukuhani wa Melkizedeki. Wazee wanapaswa kuwafundisha waumini wa Kanisa na kuwachunga.
Wazee pia huitwa kwenda kwenye misheni kufundisha injili kwa watu ulimwenguni kote.
Wanaume wote ambao wana Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kubariki watu. Wanaweza pia kuwapa watu Roho Mtakatifu.
Ukuhani mwingine ni Ukuhani wa Haruni, ambao pia unaitwa ukuhani mdogo. Ukuhani wa Haruni unajumuisha ofisi za askofu, kuhani, mwalimu, na shemasi. Makuhani wanaweza kubatiza watu, kubariki sakramenti, na kuwasaidia wazee.
Walimu huandaa sakramenti. Wanafanya mafundisho ya nyumbani na kusaidia waumini wa Kanisa kuishi maisha mema.
Mashemasi wakipitisha sakramenti. Wao pia hukusanya sadaka ya mfungo na kumsaidia askofu.
Yesu alisema watu wote ambao wana ukuhani wanapaswa kujifunza yale Mungu anayotaka wafanye. Ikiwa watafanya kazi kwa bidii, Baba wa Mbinguni atawabariki.