Hadithi za Maandiko
Sura ya 11: Watu Zaidi Wanajiunga na Kanisa: Aprili–Juni 1830


Sura ya 11

Watu Zaidi Wanajiunga na Kanisa

Aprili–Juni 1830

ubatizo
waumini wanawasili

Baada ya wiki chache, kulikuwa na waumini 27 wa Kanisa. Wote hawakuishi katika mji mmoja. Joseph Smith aliwaomba waje kwenye mkutano, ambao ni mkutano maalum kwa ajili ya Watakatifu wote. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo wanaitwa Watakatifu.

Watakatifu wakipokea sakramenti

Watakatifu walishiriki sakramenti katika mkutano. Baadhi ya wanaume walitawazwa kwenye ukuhani. Roho Mtakatifu aliwabariki Watakatifu, na walikuwa na furaha tele.

watu wakihudhuria mkutano

Baadhi ya watu wengine waliohudhuria mkutano hawakuwa waumini wa Kanisa. Walijifunza kuhusu injili na walitaka kujiunga na Kanisa, hivyo wakabatizwa. Baada ya mkutano, Joseph Smith alikwenda mji mwingine. Watu wengine huko pia walitaka kubatizwa. Joseph alisema wangeweza kubatizwa katika mto uliokuwa karibu.

watu waovu wakiharibu bwawa

Watu walijenga bwawa dogo katika mto ili kufanya maji kuwa yenye kina cha kutosha kwa ajili ya kufanya ubatizo. Wakati wa usiku, baadhi ya watu waliharibu bwawa.

Kundi la watu wenye fujo likiingilia ubatizo

Bwawa lilijengwa upya, na Oliver Cowdery akaanza kubatiza watu. Mara kundi la watu wenye fujo likaja. Kundi la watu wenye fujo ni kundi la watu wenye hila. Walisema mambo mabaya na kujaribu kuwaumiza Watakatifu, lakini Bwana aliwaweka watu salama.

Joseph ndani ya chumba cha gereza

Kundi la watu wenye fujo liliendelea kujaribu kuleta matatizo kwa Kanisa. Walisema uongo kuhusu Joseph Smith na kumfanya akamatwe. Kwenye kesi, walipata watu wa kutoa ushahidi wa uongo dhidi ya Nabii. Lakini watu wengine wengi walisema ukweli kuhusu Joseph, wakithibitisha maneno ya maadui kuwa ni uongo.

Joseph akikamatwa tena

Joseph aliachiliwa, lakini haraka sana akakamatwa tena na watu kutoka wilaya ya jirani. Wakati akiwa kifungoni, watu walimtemea mate na hawakumpatia chakula. Kesi nyingine ilifanyika, na Joseph kwa mara nyingine tena hakupatikana na hatia na aliachiliwa.