Scripture Stories
Sura ya 47: Watakatifu Wanaondoka Missouri: Msimu wa Baridi 1839


Sura ya 47

Watakatifu Wanaondoka Missouri

Msimu wa Baridi 1839

Picha
wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
Picha
Brigham Young akiongoza Kanisa

Wakati Joseph Smith alipokuwa jela, mengi ya majukumu ya kuongoza Watakatifu yaliwekwa juu ya Brigham Young, mmoja wa Mitume. Alifanya mkutano ili kuwaambia Watakatifu kwamba ni lazima waanze kujiandaa ili kuondoka Missouri. Wengi wa Watakatifu walikuwa masikini na hawakuwa na magari ya kukokotwa na maksai au farasi. Wanaume katika mkutano walisema wangewasaidia Watakatifu masikini kuhama.

Picha
Watakatifu wakiondoka Missouri

Watakatifu walianza kuondoka Missouri mnamo Februari 1839, wakati ilipokuwa baridi kali. Waliambiwa kwamba watu katika jimbo la Illinois wanaweza kuwa marafiki kwao, hivyo walisafiri maili 200 kuelekea magharibi mwa Illinois. Wengi wao walikwenda katika mji wa Quincy, ambapo watu walikuwa wakarimu na waliwapa malazi, chakula, na ajira.

Picha
Gavana Boggs ana furaha

Gavana Boggs na rafiki zake walifurahia kuona Watakatifu waliondoka Missouri.

Chapisha