Sura ya 53 Matatizo katika Nauvoo Mei–Agosti 1842 Maelfu ya Watakatifu walienda kuishi Nauvoo. Walijenga mji mzuri na kuanza kujenga hekalu. Watakatifu walimchagua John C. Bennett kuwa meya wa Nauvoo. Mwanzoni alikuwa meya mzuri, lakini baadaye alianza kufanya mambo mabaya na kugeuka dhidi ya Joseph Smith. Watu katika Nauvoo walitaka kuwa na sikukuu maalum, pamoja na askari wa Kikosi cha Nauvoo wakiandamana katika gwaride. John Bennett aliamua kwamba askari walipaswa kuwa na vita ya mzaha. Hiyo ilimaanisha itakuwa ni vita ya kuigiza, sio ya kweli. Bw. Bennett alimwomba Joseph Smith kuongoza kundi moja la askari katika vita, lakini Joseph hakufanya hivyo. Roho Mtakatifu alikuwa amemwambia Joseph kwamba John Bennett alikuwa akipanga kutumia vita ili kumfanya auwawe. John Bennett alikuwa na hasira. Kwa sababu John Bennett alikuwa amegeuka dhidi ya Nabii na kufanya mambo mengine mabaya, alitengwa na Kanisa na hakuwa tena meya wa Nauvoo. Joseph Smith akawa meya mpya. John Bennett alikuwa na hasira. Aliondoka Nauvoo na kuanza kusema na kuandika mambo mabaya juu ya Joseph Smith na Kanisa. Pia alipata watu wengine wa kujiunga naye. Joseph Smith aliwaambia baadhi ya watu wa Kanisa kwamba Watakatifu watakuwa na matatizo mengi. Siku moja itabidi waondoke Nauvoo. Joseph alitabiri kwamba wataenda kwenye Milima ya Mawe na kujenga miji huko. Wataweza kumtii Mungu na kuwa watu wenye nguvu.