Scripture Stories
Sura ya 65: Kanisa la Yesu Kristo Leo


Sura ya 65

Kanisa la Yesu Kristo Leo

Picha
kuelekea magharibi
Picha
Joseph Smith pamoja na akina kaka

Miaka mingi imepita tangu Kanisa lilipoanzishwa huko Fayette, New York. Kanisa limekuwa kubwa sana katika miaka hiyo. Mnamo 1830 lilianza na waumini sita pekee.

Picha
Wamisionari wakisalimiana na tamaduni mbali mbali

Tangu 1830, wamisionari wamekwenda kote ulimwenguni wakifundisha injili. Watu wamewasikiliza wamisionari na kujiunga na Kanisa. Leo mamilioni ya waumini wa Kanisa wanaishi ulimwenguni kote. Wanazungumza lugha nyingi. Ingawa waumini wanaishi katika maeneo mbalimbali, Kanisa ni lile lile. Watu wanafurahia kuwa waumini wa Kanisa.

Picha
manabii wa siku za leo wakizungumza katika mkutano

Manabii walio hai wanaendelea kuongoza Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wanapokea ufunuo kutoka kwa Yesu.

Picha
familia ikipanda bustani pamoja

Washiriki wa Kanisa wanapowafuata manabii, wanakuwa watu bora, wenye furaha zaidi. Wanakuwa na nyumba na familia imara. Wanashiriki injili na wengine. Wanawasaidia majirani zao na wengine wenye shida.

Picha
Familia imevalia mavazi meupe

Waumini wa Kanisa pia huwafuata manabii kwa kwenda hekaluni. Kanisa limejenga mahekalu kote ulimwenguni. Waumini huenda hekaluni ili kujifunza jinsi ya kuwa zaidi kama Yesu. Wanapokea ibada takatifu na kufanya maagano na Mungu. Hekaluni ni mahali pekee ambapo waumini wanaweza kufunga ndoa ya muda na ya milele. Tunabarikiwa katika njia nyingi kwa kuwa waumini wa kanisa la Bwana. Tunapaswa kushukuru kwa baraka hizi. Tunaweza kuonyesha shukrani zetu kwa kutii amri za Mungu na kuwatumikia wengine.

Chapisha