Sura ya 50 Watakatifu katika Nauvoo Januari–Julai 1841 Watakatifu walikuwa wanajenga Nauvoo kuwa mji mzuri. Mji ulikua haraka wakati waumini wapya wa Kanisa walipokusanyika huko kutoka Uingereza na maeneo mengine. Yesu alimpa Joseph Smith ufunuo muhimu kuhusu kile Watakatifu walichopaswa kufanya katika Nauvoo. Mafundisho na Maagano 124 Yesu alimwambia Joseph Smith kuandika barua akiwaambia wafalme wote na viongozi duniani kuhusu injili iliyorejeshwa. Yesu pia alisema Watakatifu walipaswa kujenga hekalu katika Nauvoo. Aliwataka kuleta dhahabu, fedha, vyuma vingine, na aina nyingi za mbao nzuri ili kujenga hekalu. Mafundisho na Maagano 124:1–8, 26–27 Yesu alisema Angekuja hekaluni. Huko Angetoa Ufunuo kuhusu ukuhani. Pia Angerejesha ibada na kufunua maarifa zaidi. Mafundisho na Maagano 124:27–31, 40–41 Yesu alimwambia Joseph kuwa Watakatifu wangeweza kubatizwa kwa ajili ya watu ambao wamekufa. Yesu alisema Watakatifu walipaswa kujenga kisima cha ubatizo ndani ya hekalu ambapo wangeweza kubatizwa kwa ajili ya wafu. Mafundisho na Maagano 124:29–37 Yesu pia alifunua kwamba Hyrum Smith, kaka yake Joseph, alipaswa kuwa patriaki wa Kanisa. Kama patriaki, Hyrum angetoa baraka maalum kwa waumini wa Kanisa. Mafundisho na Maagano 124:91–92 Yesu pia alimpa Joseph Smith ufunuo kuhusu Brigham Young. Yesu alisema alijua kuwa Brigham alifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Kanisa. Alikuwa ameacha nyumba na familia yake mara nyingi ili kutumikia misheni. Mafundisho na Maagano 126:1–2 Yesu alimwambia Brigham Young kwamba alipaswa kukaa na familia yake na kuwapa matunzo maalum. Mafundisho na Maagano 126:3