Hadithi za Maandiko
Sura ya 36: Kambi ya Sayuni: Februari–Juni 1834


Sura ya 36

Kambi ya Sayuni

Februari–Juni 1834

nyumba ya majira ya baridi
Joseph akisoma barua

Wakati watu katika Missouri walipokuwa wakiwafanya Watakatifu kuzihama nyumba zao, Joseph Smith alikuwa karibu umbali wa maili 1,000 huko Kirtland, Ohio. Aliomba ili kujua jinsi ya kuwasaidia Watakatifu huko Missouri.

Joseph akiinuka kutoka kwenye maombi

Katika ufunuo, Yesu alimwambia Joseph kuwa baadhi ya watu katika Kanisa wanapaswa kwenda Missouri ili kuwasaidia Watakatifu. Joseph Smith ilikuwa awe kiongozi wao. Bwana alitaka wanaume 500 waende.

Joseph akizungumza na Watakatifu

Joseph alimtii Bwana. Aliwaambia Watakatifu kwamba wanaume 500 walitakiwa kwenda katika nchi ya Sayuni huko Missouri. Lakini baada ya wiki chache, 100 tu ndio waliosema wangeweza kwenda.

Wanaume wakiondoka Kirtland

Wanaume 100 waliondoka Kirtland na kuanza safari ndefu ya Missouri. Kundi liliitwa Kambi ya Sayuni. Mara nyingi wanaume walitembea maili 35 kwa siku licha ya kuwa na njaa, kiu, na joto. Walikaa pamoja katika kambi wakati wa usiku.

Wanaume wakiondoka Kirtland

Njiani, wanaume 100 zaidi walijiunga nao. Lakini bado hapakuwa na wanaume wengi kama Bwana alivyotaka.

Washiriki wakimlalamikia Joseph

Washiriki wa kambi walisafiri maili 1,000. Baadhi yao walisema safari ilikuwa ngumu sana. Walinung’unika na kubishana. Walimlaumu Joseph Smith wakati walipokuwa hawana chakula cha kutosha. Walisema hakuwa kiongozi mzuri. Joseph aliwaambia watu hawa kwamba ni lazima watubu, vinginevyo wangeugua na kufa.

washiriki waadilifu wa kambi wakiwa pamoja na Joseph

Watu wengi katika kambi walikuwa waadilifu. Walimsaidia Joseph na kutii amri za Mungu.

wanaume wakipiga kambi kando ya mto

Hatimaye kambi ya Sayuni ilikaribia Jackson County, Missouri. Walipiga kambi kando ya mto.

genge la watu wenye fujo likiikaribia Kambi ya Sayuni

Washiriki wa genge la watu wenye fujo walikuwa wamepeleleza kambi na kujua mahali ilipokuwa. Wakati wa usiku genge la watu wenye fujo lilikuja karibu na kambi na kupanga kuishambulia.

Mvua ya mawe ikilinyeshea genge ovu la watu wenye fujo

Mungu aliilinda Kambi ya Sayuni kwa kutuma dhoruba kubwa. Upepo uliangusha miti. Mvua kubwa ya mawe ilinyesha kutoka mawinguni, na radi ilipiga miti. Mto ulijaza nchi kwa maji. Mtu mmoja katika genge la watu wenye fujo aliuawa kwa radi, na watu wengine katika genge walijeruhiwa na dhoruba. Hakuna mtu katika Kambi ya Sayuni aliyejeruhiwa.

genge la watu wenye fujo likikimbia

Wanaume katika genge la watu wenye fujo walikuwa na hofu na walikimbia. Hawakumdhuru mtu yeyote katika Kambi ya Sayuni.

Joseph akiomba

Siku tatu baada ya dhoruba, Bwana alimpa Joseph Smith ufunuo. Alisema Watakatifu walilazimika kusubiri ili kujenga mji wa Sayuni. Walihitajika kuwa watiifu zaidi, watoaji zaidi, na wenye umoja zaidi. Pia walihitajika kujifunza zaidi juu ya mambo ambayo Bwana alihitaji kutoka kwao.

Kambi ya Sayuni

Bwana pia aliwaambia wanaume wa Kambi ya Sayuni kwamba hawapaswi kupambana dhidi ya magenge ya watu wenye fujo ya Missouri. Baadhi ya wanaume walikasirika kuhusu hili. Walihisi kwamba safari haingekuwa na thamani ikiwa hawatapigana ili kuwasaidia Watakatifu katika Missouri.

Wanaume wa Kambi ya Sayuni wakiugua

Siku chache baadaye, wanaume wengi katika Kambi ya Sayuni walikuwa wagonjwa sana. Kumi na wanne kati yao walifariki. Nabii aliwaambia wanaume kuwa ugonjwa ungeondoka ikiwa watanyenyekea na kutubu. Ahadi hii ilitimizwa.

Joseph akizungumza na Watakatifu wa Missouri

Mwisho wa Kambi ya Sayuni, Joseph Smith alikutana na Watakatifu huko Missouri na kuchagua wanaume wa baraza kuu. Siku chache baadaye, yeye pamoja na wanaume wengi katika Kambi ya Sayuni walianza kurudi Kirtland.

Kambi ya Sayuni ikirudi Kirtland

Ingawa wanaume wa Kambi ya Sayuni hawakuwasadia Watakatifu katika Missouri, kambi ilikuwa bado ina thamani. Ilisaidia kuwaandaa Brigham Young na wengine kwa ajili ya uongozi katika Kanisa. Waliweza kuthibitisha ikiwa wangekuwa watiifu na kufanya dhabihu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Miezi michache baadaye, wengi wa wale ambao walikuwa waaminifu waliitwa kama viongozi katika Kanisa.