Sura ya 15 Misheni kwa Walamani Septemba 1830 Yesu alitaka watu wengi zaidi kusikia juu ya injili. Alitaka baadhi ya Watakatifu waende misheni. Alimwita Oliver Cowdery kwenda misheni kwa Wahindi wa Kiamerika. Wahindi hawa pia waliitwa Walamani kwa sababu baadhi yao walikuwa uzao wa Walamani katika Kitabu cha Mormoni. Mafundisho na Maagano 28:8 Yesu alitaka Walamani wasome Kitabu cha Mormoni. Alikuwa amewaahidi manabii wengi kwamba Walamani wangepata Kitabu cha Mormoni. Sasa ilikuwa ni wakati wa kutimiza ahadi hiyo. Mafundisho na Maagano 3:19–20 Kitabu cha Mormoni kinawaelezea Walamani kuhusu mababu zao walioishi mamia ya miaka iliyopita. Kinawaambia kuhusu ahadi muhimu ambazo Yesu aliwaahidi. Kinawasaidia kuamini katika Yesu. Kinawafundisha kutubu na kubatizwa. Mafundisho na Maagano 3:19–20 Baadhi ya wanaume walitaka kwenda na Oliver Cowdery kuhubiri injili kwa Walamani. Bwana alisema watatu kati ya wanaume hao wangeweza kwenda. Kwanza wamisionari walikwenda kwa baadhi ya makabila katika New York. Wamisionari waliwapa watu Kitabu cha Mormoni, lakini ni wachache wao tu waliweza kusoma. Kisha wamisionari walikwenda kuhubiri kwa baadhi ya Walamani huko Ohio. Hawa watu walikuwa na furaha kusikia kuhusu Kitabu cha Mormoni na kujifunza juu ya mababu zao. Wamisionari waliondoka Ohio na kwenda katika mji mmoja ulioitwa Independence katika Jackson County, Missouri. Kulikuwa na Walamani wengi katika Missouri. Wamisionari waliwahubiria Injili na kuwapa Kitabu cha Mormoni. Walikuwa na furaha tele na waliwashukuru wamisionari kwa ajili ya kitabu. Watu wengine katika Missouri hawakuamini injili ya urejesho wala Kitabu cha Mormoni. Waliwaambia wamisionari kukaa mbali na Wahindi. Watu walisema askari wangewafukuza wamisionari ikiwa hawakuondoka. Wakiwa wamehuzunika, wamisionari walikwenda kuwafundisha watu wengine huko Missouri. Mmoja wa wamisionari aliitwa Parley P. Pratt. Alikwenda Ohio kumwaambia Joseph Smith kile walichofanya. Parley alisema misheni yao ilikuwa nzuri na walikuwa wamefundisha Injili kwa watu wengi.