Sura ya 9 Uanzishaji wa Kanisa la Yesu Kristo Aprili 6, 1830 Joseph Smith alikuwa akiishi katika mji wa Fayette katika jimbo la New York. Yesu alimwambia Joseph ilikuwa ni wakati wa Kanisa Lake la Kweli kuwepo tena duniani. Alimwambia Joseph kuanzisha Kanisa hilo. Mafundisho na Maagano 20:1–2; 21:3 Mnamo Aprili 6, 1830, Joseph alifanya mkutano wa kuanzisha Kanisa. Oliver Cowdery, Hyrum Smith, Samuel Smith, David Whitmer, na Peter Whitmer walikuja kumsaidia. Wote walikuwa wamekwisha batizwa. Watu wengine pia walikuja kwenye mkutano. Wanaume hao waliomba kwa Baba wa Mbinguni. Joseph alimtawaza Oliver kuwa mzee katika Kanisa. Kisha Oliver akamtawaza Joseph. Joseph na Oliver walibariki sakramenti. Wakawapa watu. Joseph na Oliver waliweka mikono yao juu ya kichwa cha kila mwanamume ili kumthibitisha kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo na kumpa kipawa cha Roho Mtakatifu. Joseph na Oliver waliwatawaza baadhi ya wanaume wengine kwenye ukuhani. Watu hawa walikuwa na furaha tele. Walisema walimpenda Mungu na kuelezea jinsi Yeye alivyowabariki. Yesu alitoa ufunuo kwa Joseph Smith katika mkutano. Yesu alisema Joseph alikuwa nabii. Nabii wa kweli huongea kwa ajili ya Yesu. Wakati nabii anapoongea kwa ajili ya Yesu, waumini wa Kanisa wanapaswa kumsikiliza na kumtii. Mafundisho na Maagano 21:1, 4–5 Baada ya mkutano, watu wengi walibatizwa, wakiwemo mama na baba yake Joseph Smith. Siku nzuri iliyoje! Kanisa la Yesu Kristo lilikuwa duniani tena.