Sura ya 10 Muujiza wa Kwanza katika Kanisa Aprili 1830 Mkutano uliofuata wa Kanisa ulikuwa siku ya Jumapili, Aprili 11, 1830. Mbali na waumini wa Kanisa, watu wengine wengi walihudhuria mkutano huo. Oliver Cowdery alifundisha injili ya Yesu Kristo. Baadhi ya watu walimwamini Oliver na walitaka kujiunga na Kanisa. Walibatizwa baada ya mkutano. Shetani hakutaka watu wajiunge na Kanisa, hivyo alijaribu kuwafanya baadhi yao wajisikie vibaya. Mmoja wa watu hawa alikuwa mtu mmoja aliyeitwa Newel Knight. Joseph alimwomba Newel kusali katika mkutano, na Newel alisema angefanya hivyo. Lakini Shetani hakutaka Newel aombe. Wakati Newel alipokwenda kwenye mkutano, alisema alikuwa na hofu ya kuomba kwa sauti. Asubuhi iliyofuata, Newel Knight aliingia Msituni ili aweze kuomba peke yake. Newel alijaribu kuomba, lakini tena Shetani hakumtaka aombe, na hakuweza kuzungumza. Akawa mgonjwa na mwenye hofu, na akaenda nyumbani. Mke wa Newel alikuwa na wasiwasi juu ya mume wake na akamwomba Joseph Smith kusaidia. Joseph alitumia ukuhani kumbariki Newel na kumfukuza Shetani nje. Baada ya baraka, Newel alijisikia vizuri. Baadaye alibatizwa.