Sura ya 21 Ufunuo wa Kuishi Missouri Mei–Juni 1831 Joseph Smith alikuwa amehama kutoka New York hadi Kirtland, Ohio. Aliwaambia Watakatifu ambao bado walikuwa wanaishi New York kuhamia Ohio, na walimtii. Yesu alimwambia Joseph kwamba Watakatifu katika Ohio walipaswa kugawana ardhi yao na Watakatifu kutoka New York. Leman Copley alikuwa na ardhi kubwa, na aliahidi kuigawa. Baadhi ya Watakatifu kutoka New York walihamia katika ardhi hiyo. Mafundisho na Maagano 48:2 Lakini Leman Copley hakutimiza ahadi yake. Aliamua kwamba hakutaka Watakatifu wa New York kutumia ardhi yake. Aliwafanya waondoke, na hawakuwa na mahali pengine pa kuishi. Mafundisho na Maagano 54, kichwa cha habari cha sehemu Newel Knight alikuwa kiongozi wa kundi hili la Watakatifu. Hakujua nini cha kufanya, hivyo alikwenda kumwomba Joseph Smith msaada. Mafundisho na Maagano 54, kichwa cha habari cha sehemu Joseph aliomba, na Bwana alimwambia kwamba kundi hili la Watakatifu lilitakiwa kwenda Missouri. Mafundisho na Maagano 54:7–9 Kabla ya Watakatifu hawa kuondoka Kirtland, mkutano ulifanyika. Ulidumu kwa siku tatu. Bwana alitoa baadhi ya mafunuo muhimu kwa Joseph Smith. Bwana alimwambia Joseph kuwatawaza makuhani wakuu wa kwanza katika Kanisa. Makuhani wakuu wana Ukuhani wa Melkizedeki. Viongozi wengi wa Kanisa walitawazwa kuwa makuhani wakuu. Mafundisho na Maagano 52, kichwa cha habari cha sehemu Bwana alisema baadhi ya wanaume walipaswa kwenda kwenye misheni huko Missouri. Walipaswa kuhubiri injili njiani. Wakati mkutano ulipomalizika, wamisionari waliondoka kwenda Missouri. Mafundisho na maagano 52:9–10 Bwana alimwambia Joseph kuwa mkutano ujao wa Kanisa ungefanyika katika Missouri. Alimwambia Joseph na rafiki zake kwenda huko. Yesu aliahidi kuwaonyesha ni wapi pa kujenga mji wa Sayuni. Mafundisho na Maagano 52:1–5 (ona pia Mafundisho na Maagano 42:62)