Scripture Stories
Sura ya 52: Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama: Machi 1842


Sura ya 52

Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama

Machi 1842

Picha
Hekalu la Nauvoo
Picha
Watakatifu wakijenga hekalu Nauvoo

Watakatifu walikuwa wakijenga hekalu katika Nauvoo. Nguo za wanaume zilikuwa zikichakaa, na wanawake walitaka kuwasaidia. Mwanamke mmoja alisema angeweza kutengeneza nguo kwa ajili ya wanaume, lakini hakuwa na fedha za kununua kitambaa.

Picha
wanawake wakiwa wamekusanyika

Sarah Kimball alisema angeweza kumpa yule mwanamke baadhi ya vitambaa. Dada Kimball pia aliwaomba wanawake wengine kusaidia. Wanawake walifanya mkutano katika nyumba ya Dada Kimball na kuamua kuanzisha muungano kwa ajili ya wanawake katika Kanisa.

Picha
Eliza R. Snow akisalimiana na Joseph

Wanawake walimwomba Eliza R. Snow kuandika baadhi ya sheria kwa ajili ya muungano. Alipeleka sheria kwa Joseph Smith. Alisema sheria zilikuwa nzuri, lakini pia alisema Bwana alikuwa na mpango bora kwa ajili ya wanawake.

Picha
Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama unaanzishwa

Joseph Smith aliwaomba wanawake kuhudhuria mkutano. Alisema viongozi wa ukuhani wangewasaidia wanawake kwenye muungano wao. Emma Smith alichaguliwa kuwa kiongozi wa wanawake. Waliliita kundi lao Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama.

Picha
Joseph akizungumza na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama

Joseph Smith aliwaambia wanawake wawasaidie watu ambao walikuwa wagonjwa au masikini. Walipaswa kuwapa watu msaada wowote waliohitaji. Askofu angewasaidia wanawake kujua nini cha kufanya.

Picha
wanawake wamekutana pamoja

Wanawake walikuwa na mikutano ya kujifunza mambo waliyohitaji kujua. Walifurahi sana kwamba wangeweza kuwasaidia waumini wa Kanisa.

Picha
wanawake wakitengeneza nguo

Wanawake walitengeneza nguo kwa ajili ya wanaume waliokuwa wakijenga hekalu. Pia walitengeneza vifaa vya kutumika katika hekalu.

Picha
wanawake wakipeleka chakula kwa watu wenye shida.

Wanawake walipeleka chakula kwa watu waliokihitaji. Waliwasaidia watu waliokuwa wagonjwa na walifanya mambo mengine mengi ya kuwasaidia Watakatifu.

Picha
wanawake wakihudumu katika Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama

Wanawake wote katika Kanisa ni wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Wanawasaidia watu. Wanajifunza kuhusu injili. Wanajifunza kuhusu vitabu vizuri, muziki mzuri na sanaa nzuri. Wanajifunza jinsi ya kuimarisha familia zao. (Chanzo kwa ajili ya sura hii: Historia ya Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, 1842–1966 [1967].)

Chapisha