Sura ya 1 Joseph Smith na Familia Yake 1805–1820 Joseph Smith alizaliwa tarehe 23 Desemba 1805. Familia yake iliishi katika jimbo la Vermont huko Marekani. Baba yake Joseph Smith pia aliitwa Joseph. Jina la mama yake lilikuwa Lucy. Joseph Smith—Historia ya 1:3–4 Joseph alikuwa na kaka watano na dada watatu. Joseph Smith—Historia ya 1:4 Mama na baba wa Joseph walikuwa watu wema. Waliwapenda watoto wao na walifanya kazi kwa bidii ili kuwatunza. Wakati Joseph alipokuwa kijana mdogo, alikuwa na uvimbe mbaya sana kwenye mguu wake. Madaktari walijaribu kutibu mguu wake, lakini hawakuweza. Hyrum Smith alikuwa mmoja wa kaka wakubwa wa Joseph. Alimpenda Joseph na alisikitika kwamba mguu wa Joseph ulimuuma sana. Aliketi karibu na kitanda cha Joseph na kumsaidia ajisikie vizuri. Madaktari walitaka kuukata mguu wa Joseph, lakini mama yake hakuwaruhusu. Hivyo madaktari waliamua kukata sehemu ya mfupa. Joseph alijua mguu wake ungeuma wakati madaktari watakapoukata, lakini alikuwa na imani kwamba Baba wa Mbinguni angemsaidia. Madaktari walimtaka Joseph kunywa mvinyo kidogo ili maumivu yasiwe makali sana. Joseph alikataa kunywa mvinyo. Joseph alimwomba mama yake kwenda nje kwa sababu hakumtaka aone madaktari wakikata kwenye mguu wake. Joseph alimwomba baba yake amshikilie wakati madaktari wakikata kwenye mguu wake. Waliondoa sehemu mbaya za mfupa. Hii iliumiza sana, lakini Joseph alikuwa jasiri. Baada ya siku nyingi, mguu wake ulikuwa vizuri. Wakati Joseph alipokuwa na umri mkubwa, familia yake ilihamia jimbo la New York. Waliishi katika nyumba ya magogo kwenye shamba karibu na Palmyra. Joseph Smith—Historia ya 1:3 Familia ya Joseph ilikuwa masikini. Walifanya kazi kwa bidii kulipia shamba. Wavulana walimsaidia baba yao kupanda mazao na kutunza mifugo. Wasichana walifanya kazi na mama yao. Joseph alikuwa mtoto mzuri. Alikuwa na furaha na alipenda kucheka na kuburudika.