Sura ya 7 Mashahidi Wanaona Mabamba ya Dhahabu 1829–1830 Joseph Smith na Oliver Cowdery walimaliza kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Yesu alitaka watu wasome kitabu. Pia aliwataka wajue kwamba Joseph alikuwa amesema ukweli kuhusu mabamba ya dhahabu. Mafundisho na Maagano 17:4–5 Yesu alichagua watu wengine watatu kuona mabamba ya dhahabu na kuwa mashahidi kwamba yalikuwa halisi. Watu hawa walikuwa Martin Harris, Oliver Cowdery, na David Whitmer. Joseph aliwachukua mashahidi watatu kwenda nao msituni, ambako waliomba. Malaika alikuja na kuwaonyesha mabamba ya dhahabu. Yesu aliwataka mashahidi watatu kuwaambia watu mambo waliyoyaona. Mafundisho na Maagano 17:3, 5 “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” (ona kurasa za utangulizi za Kitabu cha Mormoni) Joseph Smith alikuwa na furaha tele. Mashahidi watatu wangewaambia watu juu ya mabamba ya dhahabu, na watu wengi wangeamini kwamba Joseph alisema ukweli. Yesu alimwambia Joseph kuonyesha mabamba kwa mashahidi wengine wanane. Wanaume wanane walishika mabamba ya dhahabu katika mikono yao na kuona maandishi kwenye mabamba. “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” (ona kurasa za utanguliza za Kitabu cha Mormoni) Mashahidi wote waliandika juu ya mabamba ya dhahabu. Walisema waliyaona mabamba, na walishuhudia kwamba mabamba yalikuwa halisi. Maneno ya mashahidi yako katika Kitabu cha Mormoni. “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” na “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane” (ona kurasa za utanguliza za Kitabu cha Mormoni) Baada ya Joseph Smith kutafsiri mabamba na mashahidi kuyaona, Joseph hakuyahitaji tena. Malaika Moroni alitokea, na Joseph akamrudishia mabamba ya dhahabu. Baada ya Joseph kumaliza kutafsiri Kitabu cha Mormoni, alikipeleka kwa mchapishaji. Joseph hakuwa na fedha za kumlipa mchapishaji. Martin Harris alikuwa na fedha za kutosha, na katika ufunuo aliombwa kuzitoa ili kumlipa mchapishaji. Mafundisho na Maagano 19:26, 35 Shetani hakutaka Kitabu cha Mormoni kichapishwe. Hakutaka watu wakisome. Watu waovu walijaribu kuzuia uchapishaji. Mtu mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha uchapishaji Jumapili na kuiba baadhi ya kurasa za Kitabu cha Mormoni. Alichapisha kurasa katika gazeti mpaka pale watu wengine walipomzuia kuziiba. Watu waliojaribu kuzuia uchapishaji hawakufanikiwa kwa sababu wale ambao ni waovu hawawezi kuzuia kazi ya Yesu. Baada ya miezi mingi, uchapishaji wa Kitabu cha Mormoni ulikamilika.