Hadithi za Maandiko
Mandhari kutoka katika Historia ya Kanisa


Mandhari kutoka katika Historia ya Kanisa

Kijisitu Kitakatifu

Kijisitu Kitakatifu. Katika miti hii karibu na nyumba yake, Nabii Joseph Smith alipokea Ono la Kwanza.

nyumba ya magogo ya Joseph Smith Mkubwa

Nyumba ya magogo ya Joseph Smith Mkubwa Huu ni mfano wa nyumba ambayo familia ya Smith iliwahi kuishipo.

Mtambo wa uchapishaji wa Grandin

Mtambo wa Grandin na Kiwanda cha Uchapishaji. Uchapishaji wa kwanza wa Kitabu cha Mormoni ulifanyika hapa.

Mto Susquehanna

Mto Susquehanna. Ukuhani wa Haruni na Ukuhani wa Melkizedeki ulirejeshwa katika kingo za mto huu (ona Mafundisho na Maagano 13; 128:20).

nyumba ya magogo ya Peter Whitmer Mkubwa

Nyumba ya magogo ya Peter Whitmer Mkubwa Nyumba inayofanana na hii ilijengwa kwenye eneo ambapo Kanisa lilianzishwa mnamo tarehe 6 Aprili 1830.

Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland. Hili lilikuwa hekalu la kwanza kujengwa katika siku hizi za mwisho. Yesu, Musa, Elia, na Eliya walirejesha funguo za ukuhani katika hekalu hili.

Adam-ondi-Ahman

Bonde la Adam‑ondi-Ahman. Adamu, manabii wengine, na Watakatifu waaminifu watakutana na Mwokozi hapa kabla ya Ujio Wake wa Pili.

Jela ya liberty

Jela ya liberty. Wakati akiwa amefungwa hapa kinyume na sheria, Joseph Smith alipokea ufunuo ambao sasa umeandikwa katika Mafundisho na Maagano 121–23.

Hekalu la Nauvoo

Hekalu la Nauvoo Illinois. Hekalu la Nauvoo, ambalo liliharibiwa baada ya Watakatifu kuhama mji mnamo 1846, lilijengwa upya na kuwekwa wakfu mnamo 2002.

Nyumba ya Brigham Young

Nyumba ya Brigham Young. Hii ni picha ya nyumba iliyojengwa upya ya Brigham Young katika Nauvoo, Illinois.

Watakatifu wakielekea magharibi

Watakatifu Wakielekea Magharibi. Mchoro na C. C. A. Christensen

Hekalu la Salt Lake

Hekalu la Salt Lake. Hekalu la Salt Lake liliwachukua Watakatifu miaka 40 kulijenga.