Scripture Stories
Sura ya 40: Maono katika Hekalu la Kirtland: Aprili 1836


Sura ya 40

Maono katika Hekalu la Kirtland

Aprili 1836

Picha
wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
Picha
Mitume wakibariki sakramenti

Wiki moja baada ya Hekalu la Kirtland kuwekwa wakfu, Watakatifu walifanya mkutano mwingine huko. Mitume walibariki sakramenti, na Joseph Smith na washauri wake walipitisha sakramenti kwa Watakatifu.

Mafundisho na Maagano 110, kichwa cha habari cha sehemu

Picha
Yesu akiwatokea Joseph na Oliver

Kisha Joseph Smith na Oliver Cowdery waliingia mahali pa peke yao katika hekalu, ambapo walipiga magoti na kuomba. Baada ya maombi yao, walipata ono la kustaajabisha. Walimwona Bwana Yesu Kristo. Macho yake yalikuwa angavu, kama moto. Nywele zake zilikuwa nyeupe kama theluji, na uso Wake uling’ara kuliko jua.

Picha
Yesu analikubali hekalu

Yesu aliwaambia Joseph na Oliver mambo mengi ya kupendeza. Aliwaambia wawe na furaha kwa sababu dhambi zao zilikuwa zimesamehewa. Alikuwa amefurahishwa na hekalu na alisema Watakatifu waliolijenga wanapaswa kuwa na furaha. Alilikubali hekalu kama nyumba Yake takatifu. Yesu alisema angekuja hekaluni mara nyingi. Lakini kama watu hawataliweka hekalu kuwa takatifu, Yeye asingekuja.

Picha
Musa akimtokea Joseph na Oliver

Kisha Joseph na Oliver walimwona Musa hekaluni. Musa alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Alirudi duniani ili kurejesha nguvu maalum za ukuhani kwa Joseph na Oliver. Nguvu hii ingewasaidia wana wa Israeli kukusanyika katika Kanisa kutoka sehemu zote za dunia. Nguvu hii pia inampa nabii mamlaka ya kutuma wamisionari kuhubiri Injili ulimwenguni kote.

Picha
Elia akijitokeza kwa Joseph na Oliver

Kisha, Joseph na Oliver walimwona Elia. Elia aliwarejeshea nguvu maalum ya ukuhani ambayo ilikuwa imetolewa kwa Ibrahimu. Ibrahimu pia alikuwa nabii aliyeishi hapo kale. Kwa nguvu hii, Watakatifu wangeweza kuwa na baraka hizo maalum ambazo Mungu alimwahidi Ibrahimu.

Picha
Eliya anajitokeza kwa Joseph na Oliver

Kisha Joseph na Oliver walimwona Eliya, nabii mwingine aliyeishi hapo kale. Eliya alirejesha kwao nguvu maalum ya ukuhani ili kuzisaidia familia za wenye haki. Nguvu hii huziwezesha familia kuunganishwa pamoja hekaluni ili waweze kuishi pamoja milele.

Chapisha