Sura ya 14 Nabii na Ufunuo kwa ajili ya Kanisa Septemba 1830 Joseph na Emma Smith walihamia tena New York. Mtu mmoja aliyeitwa Hiram Page aliishi huko. Alikuwa muumini wa Kanisa. Alikuwa na jiwe ambalo alisema lilimsaidia kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa. Mafundisho na Maagano 28, kichwa cha habari cha sehemu Waumini wengi wa Kanisa walimwamini Hiram Page, akiwemo Oliver Cowdery. Baadhi ya watu walidhani Hiram Page alikuwa nabii. Mafundisho na Maagano 28, kichwa cha habari cha sehemu Oliver alimwuliza Joseph kuhusu Hiram Page. Joseph aliomba, na Yesu alimpa ufunuo. Yesu alisema kwamba mtu mmoja tu ndiye angeweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote. Mtu huyo alikuwa Nabii Joseph Smith. Mafundisho na Maagano 28:2 Yesu alisema kwamba Oliver na wengine wangeweza kupokea ufunuo kwa ajili yao wenyewe, lakini si kwa ajili ya Kanisa lote. Oliver alimwamini Joseph. Alijua kwamba ufunuo wa Hiram Page haukuwa sahihi. Mafundisho na Maagano 28:4–5, 8 Yesu alimwambia Oliver kuzungumza na Hiram Page. Oliver alimwambia kwamba ufunuo aliopokea kupitia jiwe haukutoka kwa Mungu. Mafundisho na Maagano 28:11 Oliver alisema kwamba Shetani alikuwa amemdanganya Hiram Page. Hiram alimsikiliza Oliver na alitubu. Mafundisho na Maagano 28:11 Leo ni Rais wa Kanisa pekee ndiye anayepokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote. Yeye ni nabii wa Mungu. Waumini wa Kanisa wanapaswa kumtii nabii.