Scripture Stories
Sura ya 23: Mafundisho na Maagano: Agosti–Novemba 1831


Sura ya 23

Mafundisho na Maagano

Agosti–Novemba 1831

Picha
gari la kukokotwa na maksai
Picha
Joseph akiondoka Missouri

Joseph Smith na baadhi ya Watakatifu waliondoka Missouri na kurudi Kirtland, Ohio. Punde mkutano maalum ulifanyika. Lengo lilikuwa ni kuzungumza kuhusu kuchapisha mafunuo ya Bwana aliyokuwa amempa Joseph Smith.

Mafundisho na Maagano 67, kichwa cha habari cha sehemu

Picha
Joseph akiandika mafunuo

Mafunuo ambayo Joseph alikuwa amepokea yalikuwa yameandikwa, lakini waumini wengi wa Kanisa hawakuwa na nakala zake. Katika mkutano, Watakatifu waliamua kuchapisha mafunuo hayo katika kitabu. Kitabu kingeitwa Kitabu cha Amri. Baadaye kiliitwa Mafundisho na Maagano.

Picha
Joseph akizungumza na muumini

Yesu alimpa Joseph Smith mafunuo mengine mawili kwa ajili ya kitabu. Mmoja ulikuwa kwa ajili ya mwanzo, na mwingine kwa ajili ya mwisho. Ufunuo huu unatusaidia kuelewa umuhimu wa kitabu na wa injili iliyorejeshwa.

Mafundisho na Maagano 67:4

Mafundisho na Maagano 67 na 133, vichwa vya habari vya sehemu

Picha
kanisa la siku za leo

Mafundisho na Maagano inamwambia kila mtu kwamba Kanisa la kweli la Yesu Kristo lipo tena duniani.

Picha
wenye ukuhani wakitoa baraka

Mafundisho na Maagano inaelezea kuhusu ukuhani. Pia inawaelezea wanaume jinsi ya kutumia uwezo huu.

Picha
wenza wakisoma kutoka katika Kitabu cha Mormoni

Mafundisho na Maagano inaelezea kuhusu Kitabu cha Mormoni. Kwa kusoma Kitabu cha Mormoni, kila mtu anaweza kujua kuhusu injili ya Yesu Kristo.

Picha
akina dada wakishiriki chakula

Mafundisho na Maagano inafundisha Watakatifu kushiriki. Wale wanaoshiriki watajazwa na Roho Mtakatifu.

Picha
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Mafundisho na Maagano inafundisha amri za Mungu. Watakatifu wanaotii amri hizi wanaweza kuishi na Baba wa Mbinguni na Yesu milele.

Picha
watu wakisoma Mafundisho na Maagano

Yesu alisema waumini wote wa Kanisa wanapaswa kusoma Mafundisho na Maagano.

Picha
Joseph kwenye kiwanda cha uchapishaji

Baada ya mkutano, Oliver Cowdery alipeleka nakala za mafunuo huko Missouri. Alimpa William Phelps, muumini wa Kanisa aliyekuwa na kiwanda cha uchapishaji. Oliver alimwomba Ndugu Phelps kuchapisha vitabu 3,000. Kabla ya uchapishaji kukamilika, hata hivyo, watu waovu walisimamisha uchapishaji na kuharibu kurasa nyingi.

Picha
msichana akiwa ameshikilia Mafundisho na Maagano

Mafundisho na Maagano hatimaye ilichapishwa mnamo 1835. Watakatifu walimshukuru Baba wa Mbinguni kwa mafunuo yaliyomo katika Mafundisho na Maagano.

Chapisha