Sura ya 44 Zaka Julai 1838 Bwana alikuwa amemwambia Joseph Smith kwamba waumini wa Kanisa wanapaswa kulipa zaka. Wakati Joseph alipokuwa Far West, Missouri, aliomba ili kuuliza ni kiasi gani cha zaka Watakatifu wanapaswa kulipa. Bwana alifunua kuwa Watakatifu wanapaswa kulipa moja ya kumi ya vyote waliyokuwa navyo kwa ajili ya zaka. Mafundisho na Maagano 119, kichwa cha habari cha sehemu Mafundisho na Maagano 64:23; 119:3–4 Kama walipata senti 10, walipaswa kutoa senti moja kwa ajili ya zaka. Kama walipata senti 100, walipaswa kutoa senti 10. Watakatifu walilipa zaka katika njia zingine pia. Walitoa moja ya kumi ya mazao waliyopanda, kama vile nafaka na nyasi za kulishia mifugo. Pia walitoa moja ya kumi ya kuku zao na wanyama wengine. Pia walilipa zaka kwenye maziwa na mboga. Zaka hutumika kujenga na kutunza mahekalu, nyumba za ibada, na majengo mengine ya Kanisa. Zaka pia hutumika kusaidia katika kazi ya umisionari. Aidha, inatumika kusaidia kulipia kutafsiri na kuchapisha maandiko na nyenzo zingine za Kanisa. Zaka inatumika kuwasaidia waumini wa Kanisa. Zaka na matoleo mengine hutumika kusaidia kununua chakula na nguo kwa ajili ya watu wenye uhitaji. Bwana anatarajia kila mmoja wetu alipe zaka kamili. Tunatoa zaka yetu kwa askofu. Yeye huituma kwenye ofisi kuu za Kanisa, ambapo nabii na viongozi wengine wa Kanisa kwa maombi huamua jinsi inavyopaswa kutumika. Mafundisho na Maagano 120 Baba wa Mbinguni anatoa baraka za kupendeza kwa Watakatifu ambao hulipa zaka. Watakatifu wasiolipa zaka hawawezi kuwa na baraka hizi zote. Biblia inasema kwamba Watakatifu wasiolipa zaka wanamwibia Mungu. Malaki 3:8–10.