Hadithi za Maandiko
Sura ya 46: Joseph Smith katika jela ya Liberty: Novemba 1838–Aprili 1839


Sura ya 46

Joseph Smith katika jela ya Liberty

Novemba 1838–Aprili 1839

wanandoa katika gari la kukokotwa na maksai
Joseph na marafiki wakipelekwa jela ya Liberty

Joseph Smith na rafiki zake walifungwa gerezani kwa siku nyingi huko Richmond, Missouri. Kisha walipelekwa jela huko Liberty, Missouri.

Joseph na marafiki katika jela ya Liberty

Joseph na rafiki zake waliwekwa katika jela ya Liberty kwa zaidi ya miezi minne. Waliteseka sana. Jela lilikuwa la baridi na chafu, na wakati mwingine walifungwa kwa minyororo. Iliwabidi kulala kwenye sakafu.

Joseph akiwa amemshikilia rafiki mgonjwa

Chakula hakikuwa kizuri. Wakati mwingine kiliwekewa sumu na kuwafanya waumwe.

Joseph akiwa na wasiwasi

Joseph alihuzunika. Hakujua kama yeye na rafiki zake wangeweza kutoka nje ya jela. Alikuwa na wasiwasi juu ya familia yake na waumini wa Kanisa.

Joseph akiomba

Joseph aliomba kumwuliza Baba wa Mbinguni ni kwa muda gani yeye na Watakatifu wangeendelea kuteseka. Pia alimwomba Baba wa Mbinguni awasaidie.

Joseph akipata ono la marafiki zake

Kwa kujibu ombi hili, Yesu alimwambia Joseph awe na amani. Alisema matatizo ya Joseph yangedumu kwa muda mfupi tu. Yesu pia alisema kwamba kama Joseph atakuwa mwaminifu, Mungu angembariki. Yesu alimwambia Joseph kwamba rafiki zake bado walimpenda na kwamba muda si mrefu angekuwa pamoja nao.

mwanamume akifariki kwenye mapigano

Yesu alisema kwamba watu waovu walio waumiza Watakatifu wataadhibiwa. Wao na watoto wao watateseka. Wasingepata ukuhani.

Joseph akipata ono la Watakatifu

Yesu alimwambia Joseph kwamba mambo mengi mazuri yatatokea kwa Watakatifu. Hakuna kitakachoweza kumzuia Mungu kuwabariki. Roho Mtakatifu angewafundisha mambo ya kupendeza kuhusu mbingu na dunia.

Joseph akiona ono la dhabihu ya Kristo

Yesu alisema Joseph hapaswi kuwa na hofu juu ya kile wanadamu wanachoweza kumfanyia. Yesu alisema matatizo na mateso yanaweza kuwa kwa faida yetu kwa sababu yanatusaidia kujifunza. Yesu alimkumbusha Joseph kwamba Yeye ameteseka zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Yesu alimtia moyo Joseph kuwa mwaminifu na aliahidi kwamba Mungu angekuwa pamoja naye.