Scripture Stories
Sehemu za Kujua


Sehemu za Kujua

Adam-ondi-Ahman

Adam-ondi-Ahman ni mahali katika jimbo la Missouri. Yesu alimtembelea Adamu huko miaka mingi iliyopita.

Amerika

Amerika ni nchi ambapo watu wa Kitabu cha Mormoni waliishi miaka mingi iliyopita.

Arizona

Arizona ni jimbo katika magharibi ya Marekani. Brigham Young aliwatuma Watakatifu kujenga miji katika Arizona.

California

California ni jimbo katika magharibi ya Marekani. Brigham Young aliwatuma Watakatifu kujenga miji katika California.

Carthage

Carthage ni mji katika Illinois. Joseph na Hyrum Smith waliuawa katika jela ya Carthage.

ufalme wa selestia wa mbinguni

Ufalme wa selestia wa mbinguni ni mahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu wanaishi. Watakatifu wenye haki wataishi huko baada ya kufufuka kwao.

Colorado

Colorado ni jimbo katika magharibi ya Marekani.

Council Bluffs

Council Bluffs ni mji katika uwanda wa Marekani. Unapatikana katika Iowa.

Misri

Misri ni nchi ambayo Ibrahimu na Musa waliishi miaka mingi iliyopita.

Far West

Far West ulikuwa mji katika jimbo la Missouri. Watakatifu waliishi katika Far West kwa muda.

Fayette

Fayette ni mji katika jimbo la New York. Joseph Smith alianzisha Kanisa huko Fayette.

Bustani ya Gethsemane

Bustani ya Gethsemane ipo karibu na Yerusalemu. Yesu aliteswa na kumwaga damu kwa ajili yetu katika Bustani ya Gethsemane.

Bonde Kuu la Salt Lake

Bonde Kuu la Salt Lake lipo magharibi ya Marekani.

Harmony

Harmony ni mji katika Pennsylvania ambapo Joseph Smith aliishi.

Haun’s Mill

Haun’s Mill ulikuwa mji katika Missouri. Genge la watu wenye fujo liliwaua Watakatifu wengi katika Haun’s Mill.

mbinguni

Mbinguni ni mahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu wanaishi. Tuliishi mbinguni kabla ya kuja duniani.

Kilima Kumora

Kilima Kumora kilikuwa karibu na nyumba ya Joseph Smith huko New York. Mabamba ya dhahabu yalizikwa katika Kilima Kumora.

Idaho

Idaho ni jimbo katika magharibi ya Marekani. Brigham Young aliwatuma Watakatifu kujenga miji katika Idaho.

Illinois

Illinois ni jimbo katika magharibi ya kati ya Marekani. Nauvoo na Carthage ni miji katika Illinois.

Independence

Independence ni mji katika Jackson County, Missouri. Yesu alisema kuwa mji wa Sayuni utajengwa karibu na Independence.

Jackson County

Jackson County ipo Missouri. Magenge ya watu wenye fujo yalifanya Watakatifu waondoke Jackson County.

Yerusalemu

Yerusalemu ni mji katika Israeli. Yesu atakwenda Yerusalemu wakati atakapokuja tena duniani.

Kirtland

Kirtland ni mji katika Ohio. Watakatifu wa mwanzo waliishi Kirtland kwa miaka kadhaa na kujenga hekalu huko.

Liberty

Liberty ni mji katika Missouri. Joseph Smith alikuwa katika Jela ya Liberty kwa miezi kadhaa.

Mto Mississippi

Sehemu ya Mto Mississippi ipo karibu na mji wa Nauvoo. Watakatifu walivuka mto Mississippi wakati walipoondoka Nauvoo.

Missouri

Missouri ni jimbo katika magharibi ya kati ya Marekani. Independence ni mji katika Missouri.

Nauvoo

Nauvoo ni mji katika Illinois. Watakatifu waliishi Nauvoo na walijenga hekalu huko.

New York

New York ni jimbo katika mashariki ya Marekani. Kilima Kumora kipo New York. Palmyra na Fayette ni miji katika New York.

Ohio

Ohio ni jimbo katika magharibi ya kati ya Marekani. Kirtland ni mji katika Ohio.

Bahari ya Pasifiki

Bahari ya Pasifiki iko upande wa magharibi mwa Marekani. Kikosi cha Mormoni kiliandamana kuelekea Bahari ya Pasifiki.

Palmyra

Palmyra ni mji katika New York ambapo familia ya Joseph Smith iliishi kwa miaka mingi.

Pennsylvania

Pennsylvania ni jimbo katika mashariki ya Marekani. Familia ya Emma Smith iliishi Pennsylvania.

Pueblo

Pueblo ni mji katika Colorado. Wanaume katika Kikosi cha Mormoni waliacha familia zao huko Pueblo.

Quincy

Quincy ni mji katika Illinois.

Milima ya Miamba

Milima ya Miamba inapatikana katika sehemu ya magharibi ya Marekani. Waanzilishi walivuka Milima ya Miamba na kwenda katika Bonde Kuu la Salt Lake.

Mji wa Salt Lake

Waanzilishi walijenga Mji wa Salt Lake. Unapatikana katika Bonde Kuu la Salt Lake.

ufalme wa telestia wa mbinguni

Watu ambao si wema duniani wataishi katika ufalme wa telestia wa mbinguni baada ya kufufuka.

ufalme wa terestria wa mbinguni

Watu ambao ni wema lakini hawatii amri zote za Mungu duniani wataishi katika ufalme wa terestria wa mbinguni baada kufufuka.

Marekani

Marekani ni nchi katika Amerika ya Kaskazini. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho lilirejeshwa huko Marekani.

Utah

Utah ni jimbo katika magharibi ya Marekani. Mji wa Salt Lake upo Utah.

Vermont

Vermont ni jimbo katika mashariki ya Marekani. Joseph Smith alizaliwa Vermont.

winter quarters

winter quarters ulikuwa mji katika uwanda wa Marekani.

Wyoming

Wyoming ni jimbo katika magharibi ya Marekani. Brigham Young aliwatuma Watakatifu kujenga miji katika Wyoming.

Sayuni

Sayuni ulikuwa ni mji ambao Henoko alijenga. Siku moja kutakuwa na mji mwingine utakaoitwa Sayuni. Utakuwa katika Jackson County, Missouri.

Chapisha