Maneno ya Kufahamu
-
asiliwaJoseph na Emma Smith waliasili watoto mapacha. Hii inamaanisha Joseph na Emma waliwafanya watoto mapacha kuwa sehemu ya familia yao.
-
kileoKileo si kizuri kwetu kunywa. Bia na mvinyo zina kileo ndani yake.
-
mababu Mababu zetu ni watu katika familia yetu ambao waliishi kabla yetu.
-
malaika Malaika ni mmoja wa wasaidizi wa Mungu. Malaika Moroni alizungumza na Joseph Smith.
-
Mtume Mtume ni kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Yesu alimwambia Joseph Smith kuwa Alitaka Mitume. Kumi na Wawili.
-
kukamatwaAskari walimkamata Joseph Smith Hii inamaanisha askari walimkamata na kumweka jela.
-
kushambuliwaGenge la watu wenye fujo liliwashambulia Watakatifu. Hii inamaanisha genge hilo lilianza kuwapiga Watakatifu.
-
kisima cha maji ya ubatizoKuna visima vya maji ya ubatizo katika makanisa na mahekalu. Watu wanabatizwa katika kisima cha maji ya ubatizo.
-
kubatizwaTunapojiunga na Kanisa, tunabatizwa. Tunawekwa chini ndani ya maji na kuinuliwa tena.
-
nzuriWakati kitu kinapokuwa kizuri, tunapenda kukiangalia. Bustani ni nzuri. Hekalu ni zuri.
-
amini Kuamini inamaanisha kufikiri kitu ni cha kweli. Watu wengi wanaamini injili ya Yesu Kristo.
-
askofu Askofu ni kiongozi wa kata.
-
kulaumiwaWatu walimlaumu Joseph Smith kwa sababu ya matatizo. Hii inamaanisha kwamba watu walisema Joseph Smith alisababisha matatizo yatokee.
-
azimaWakati tunapoazima kitu, tunamwuliza mtu kama tunaweza kukitumia. Ikiwa mtu anaazima farasi wa rafiki yake, anamwuliza rafiki yake kama anaweza kumtumia. Baada ya mtu kumtumia farasi huyo, anamrudisha kwa rafiki.
-
kujigambaWalinzi wa jela walijigamba kwa kile walichokuwa wamefanya. Hii inamaanisha walikuwa na furaha kuhusu hilo na kuwaambia wengine kuhusu hilo.
-
darajaWaanzilishi walivuka mto juu ya daraja.
-
tarumbeta ndogo Tarumbeta ndogo ni aina ya pembe.
-
zikwaMoroni alizika mabamba ya dhahabu. Aliyaweka katika sanduku la jiwe chini ya ardhi na kuyafunika.
-
kapteni Kapteni ni kiongozi. Kapteni Allen alikuwa kiongozi wa askari.
-
kamatwaAskari walimkamata Joseph Smith. Hii inamaanisha askari walimshika Joseph Smith na hawakumwachilia aende.
-
chaguziBaba wa Mbinguni anaturuhusu tufanye chaguzi. Hii inamaanisha Baba wa Mbinguni anaturuhusu tuamue kile tutakachofanya.
-
chaguaMungu huturuhusu kuchagua kuwa wema au waovu. Tunawachagua watu kuwa viongozi. Mungu alimchagua Brigham Young kuwaongoza Watakatifu.
-
amriWatu wema hutii amri za Mungu. Watu wema hufanya kile Mungu anachotaka wafanye.
-
mkutano Mkutano ni mkusanyiko mkubwa. Waumini wengi wa Kanisa wanakwenda kwenye mkutano.
-
washauriWashauri ni watu ambao humsaidia kiongozi. Nabii wa Kanisa ana washauri.
-
agano Agano ni ahadi. Tunapofanya agano na Mungu, tunamwahidi kwamba tutafanya kitu fulani.
-
kuumbwaYesu Kristo aliumba dunia. Hii inamaanisha kwamba Yesu Kristo alitengeneza dunia.
-
mazaowaanzilishi walipanda mazao. Mazao ni pamoja na mahindi, viazi, ngano, na vitu vingine.
-
sulubiwaYesu alisulubiwa. Hii ina maanisha Yeye alipigiliwa msalabani kwa misumari na kuachwa hapo mpaka alipokufa.
-
bwawaWatakatifu walijenga bwawa kwenye mto. Bwawa linayazuia maji yasiendelee kwenda.
-
mashemasiWavulana wanaweza kuwa mashemasi wanapokuwa na umri wa miaka 12. Mashemasi wanaweza kupitisha sakramenti.
-
aliamuaEmma na Joseph walijiuliza ikiwa waende Pennsylvania au wabakie New York. Waliamua kwenda Pennsylvania.
-
weka wakfuWakati tunapoweka wakfu kitu, tunakibariki ili kitumike kwa ajili ya kazi ya Mungu. Watakatifu waliweka wakfu hekalu.
-
haribu Kuharibu inamaanisha kubomoa, kuvunja, kuchoma, au kuua. Magenge ya watu wenye fujo yaliharibu hekalu.
-
mwanafunzi Mwanafunzi ni mtu anayemfuata Yesu na kujaribu kuwa kama Yeye.
-
pata Kupata inamaanisha kupata kitu kwa kukifanyia kazi.
-
wazeeWazee ni wanaume ambao wana ukuhani.
-
endaumenti Endaumenti ni ahadi maalum au zawadi kutoka kwa Mungu .
-
adui Adui ni mtu ambaye anamchukia mtu mwingine. Maadui wa Joseph Smith walijaribu kumuua.
-
toroka Kutoroka inamaanisha kwenda mbali na mtu au kitu. Joseph Smith alilitoroka genge la watu wenye fujo.
-
uovuUovu ni kitu kibaya sana. Shetani ni roho mwovu.
-
roho za waovuRoho Waovu ni roho wabaya Roho Waovu humfuata Shetani
-
waliotengwaWaumini wa Kanisa wanaofanya mambo mabaya wanaweza kutengwa. Wao sio tena waumini wa Kanisa.
-
imaniKuwa na imani ni kutumainia mambo yasiyoonekana ambayo ni ya kweli. Tuna imani katika Yesu Kristo. Hii inamaanisha tunaamini katika Yeye na kumtii Yeye.
-
mfungo Kufunga ni kushinda bila chakula au maji.
-
mileleMilele inamaanisha daima. Tunaweza kuishi na Baba wa Mbinguni milele ikiwa tutatii amri Zake.
-
samehe Kusamehe inamaanisha kusahau mambo mabaya ambayo mtu amefanya. Mungu atatusamehe ikiwa tutahuzunishwa na mambo tuliyoyafanya na kujaribu kutoyafanya tena.
-
kusanyika Kukusanyika kunamaanisha kuja pamoja katika sehemu moja. Joseph Smith aliwaambia Watakatifu wakusanyike Missouri.
-
vipawaVipawa ni vitu wanavyopewa watu. Roho Mtakatifu hutoa vipawa vya kiroho kwa watu ambao ni waadilifu.
-
injili Injili ya Yesu Kristo ni mpango wa wokovu. Inajumuisha mafundisho yote, ibada, na mamlaka kwa ajili yetu kurudi kuishi na Baba wa Mbinguni.
-
gavana Gavana ni kiongozi wa jimbo.
-
ponya Kuponya inamaanisha kuwafanya wagonjwa wapate nafuu. Newel K. Whitney alimbariki Joseph Smith, na Joseph aliponywa,
-
mwaminifuWatu ambao ni waaminifu hawasemi uongo. Watuwaaminifu hawachukui vitu ambavyo si mali yao.
-
jelaWanaume waliwekwa jela. Hii inamaanisha walifungiwa ndani ili wasiweze kutoroka.
-
kujiungaWatu walijiunga na Kanisa. Hii inamaanisha kuwa watu walibatizwa na kuwa waumini wa Kanisa.
-
lughaManeno tunayotumia kuandika au kuzungumza na watu wengine yanaitwa lugha.
-
ongoza Kuongoza watu kunamaanisha kuonyesha au kuwaambia cha kufanya. Nabii huongoza Kanisa
-
funga ndoaJoseph na Emma walifunga ndoa. Hii inamaanisha Joseph alikuwa mume wa Emma, na Emma alikuwa mke wa Joseph.
-
misheniMtume alikwenda misheni. Hii inamaanisha alikwenda kuwaambia watu kuhusu Injili ya Yesu Kristo.
-
mmisionari Mmisionari ni mtu ambaye anaenda misheni.
-
tii Kutii humaanisha kufanya kile tulichoambiwa tufanye. Tunapaswa kutii amri za Mungu.
-
bahari Bahari ni mkusanyiko mkubwa sana wa maji ya chumvi.
-
kutawazwa Kutawazwa inamaanisha kupewa ukuhani. Joseph Smith alimtawaza mwanamume. Hii inamaanisha Joseph Smith alimpa mwanamume ukuhani.
-
maksaiMaksai ni wanyama.
-
patriaki Patriaki hutoa baraka maalum kwa watu. Baba yake Joseph Smith alikuwa patriaki.
-
sumuSumu ni kitu ambacho kinaweza kuua watu kama wataila au kuinywa. Genge la watu wenye fujo lilijaribu kumfanya Joseph Smith anywe sumu.
-
omba Kuomba inamaanisha kuzungumza na Baba wa Mbinguni.
-
alihubiriJoseph Smith aliwahubiria watu. Hii inamaanisha aliwafundisha watu kuhusu Injili.
-
urais Urais wa Kanisa ni rais na washauri wake.
-
rais Rais ni kiongozi.
-
ukuhani Ukuhani ni uwezo wa Mungu.
-
makuhaniMakuhani wana ukuhani. Makuhani ni watu ambao husaidia katika Kanisa.
-
mpiga chapa Mpiga chapa ni mtu ambaye anachapisha vitabu.
-
gereza Gereza ni mahali ambapo watu wamewekwa na hawawezi kutoka nje. Gereza ni kama jela.
-
nabii Nabii huwaambia watu kile ambacho Mungu anataka wajue. Joseph Smith alikuwa nabii.
-
lindaWanaume walikuwa na bunduki ili kuwalinda watu. Hii inamaanisha wanaume walikuwa na bunduki ili kuwaweka watu salama. Bwana alimlinda Joseph Smith. Hii inamaanisha Bwana alimweka Joseph Smith salama.
-
kware Kware ni ndege.
-
tubuKama tunatenda jambo baya, tunapaswa kutubu. Hii inamaanisha tunahuzunika na kujaribu kutofanya jambo baya tena.
-
kufufukaYesu Kristo alifufuka. Hii inamaanisha kwamba baada ya Yeye kufa, Alifanywa hai tena. Watu wote watafufuka baada ya kufa.
-
ufunuoMawasiliano kutoka kwa Mungu kwenda kwa watoto wake duniani yanaitwa ufunuo. Joseph Smith alipokea ufunuo kuhusu hekalu.
-
uadilifuWatuwaadilifu hufanya kile kilicho sahihi. Hii inamaanisha wao hutii amri za Mungu.
-
Sabato Sabato ni siku ambayo sisi huenda kanisani. Hatupaswi kufanya kazi siku ya Sabato. Jumapili ni siku ya Sabato.
-
sakramentiTunapokea sakramenti kumkumbuka Yesu.
-
takatifuHekalu ni jengo takatifu. Hekalu ni mali ya Mungu.
-
Mtakatifu Mtakatifu ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo.
-
okoaYesu alikufa ili kutuokoa sisi. Hii inamaanisha Yesu alikufa ili sisi tuweze kurudi kuishi na Baba wa Mbinguni.
-
maandiko Maandiko ni vitabu vinavyotuambia kuhusu Mungu. Biblia, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu ni maandiko ya Kanisa.
-
shiriki Kushiriki maana yake ni kutoa sehemu ya kitu tulichonacho na kumpa mwingine.
-
askariAskari wanapigana katika jeshi.
-
roho Roho hana mwili wa nyama na mifupa.
-
iba Kuiba inamaanisha kuchukua kitu kisicho chako. Magenge ya watu wenye fujo yaliiba mifugo ya Watakatifu. Hii inamaanisha magenge ya watu wenye fujo yalichukua mifugo.
-
teseka Tunateseka tunapoumia. Joseph Smith na marafiki zake waliteseka jela.
-
apa Kuapa maana yake ni kusema maneno mabaya.
-
aliapaWalinzi wa jela waliapa. Walinzi wa jela walisema maneno mabaya.
-
lamiLami inanata na ni nyeusi.
-
hekalu Hekalu ni nyumba ya Mungu.
-
jaribuShetani anajaribu kutupa majaribu sisi. Hii inamaanisha anajaribu kutufanya sisi tufanye mambo ambayo ni mabaya.
-
zakazaka ni pesa tunayotoa kwa Mungu.
-
tumbakuTumbaku ni kitu kisichofaa kwetu. Baadhi ya watu huvuta na kutafuna tumbaku.
-
iliyotafsiriwaJoseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni katika lugha ya Kiingereza.
-
ukweliYesu anafundisha watu ukweli. Hii inamaanisha Yesu anafundisha watu kile kilicho sahihi.
-
ushuhuda ushuhuda ni hisia kwamba injili ni ya kweli.
-
watega wanyamaWatega wanyama ni watu wanaowakamata wanyama wamwituni Wao huuza manyoya ya wanyama.
-
ono Ono ni kitu ambacho Mungu huturuhusu kuona. Joseph Smith alimwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika ono.
-
mashahidiMashahidi huona kitu na kuwaambia wengine kuhusu kitu hicho. Mashahidi waliona mabamba ya dhahabu na kuwaambia wengine kuwa mabamba yalikuwa halisi.
-
abudu Kuabudu humaanisha kupenda na kutii. Shetani alitaka Musa amwabudu yeye. Tunapaswa kumwabudu Mungu.
-
jeraha Jeraha ni sehemu katika mwili wa mtu iliyoumizwa au kukatwa.