Sura ya 28 Nabii Joseph Anakwenda Tena Missouri Machi–Mei 1832 Joseph Smith alipokea ufunuo ambapo Yesu alisema Watakatifu walikuwa kama watoto Wake wadogo. Walikuwa bado wanajifunza. Yesu alisema wanapaswa kuwa na furaha na wenye shukrani. Yeye angekuwa kiongozi wao. Mafundisho na Maagano 78:17–18 Yesu alisema Alitaka Watakatifu kuwatunza wale ambao walikuwa masikini. Aliwataka kushirikiana na kusaidiana. Mafundisho na Maagano 78:3–6 Mara tu baada ya Joseph Smith kupokea ufunuo huu, yeye na baadhi ya marafiki zake walienda tena Missouri. Watakatifu wa Missouri walikuwa na furaha kumwona. Joseph aliwataka Watakatifu kuja kwenye mkutano ili aweze kuwaambia kuhusu ufunuo. Katika mkutano Bwana alimpatia Joseph ufunuo mwingine. Yesu alikuwa na furaha kwamba Watakatifu walikuwa wamesameheana. Kwa sababu walikuwa wamefanya hili, Alisema Yeye angewasamehe. Mafundisho na Maagano 82:1 Katika ufunuo huu Yesu pia aliwapa Watakatifu amri mpya. Alisema kwamba Alikuwa amewapa nchi ya Sayuni, na ni lazima wagawane ardhi hiyo kila mmoja. Kila mtu alipaswa kuwa na kile alichohitaji. Bwana pia aliwataka Watakatifu kuboresha vipaji vyao na kuvitumia kwa manufaa ya Kanisa. Mafundisho na Maagano 82:17–20 Baada ya mkutano, Joseph alitembelea Watakatifu katika miji mingi. Ilikuwa ni wakati wa furaha kwake. Aliwapenda Watakatifu. Katika ufunuo mwingine ambao Joseph alipokea wakati alipokuwa Missouri, Bwana alisema kwamba waume wanapaswa kuwatunza wake zao. Wazazi wanapaswa kuwatunza watoto wao. Mafundisho na Maagano 83:2, 4 Bwana pia alisema Watakatifu wanapaswa kuwatunza wanawake wasiokuwa na waume. Watakatifu lazima pia wawatunze watoto ambao hawana baba au mama. Mafundisho na Maagano 83:6 Yesu alisema Watakatifu wanapaswa kutoa chakula na vitu vingine kwa askofu ili kuweka katika ghala. Alisema Askofu anapaswa kutumia kile kilicho katika ghala ili kuwasaidia wale ambao ni masikini. Mafundisho na Maagano 83:6 Baada ya Joseph Smith kumaliza kazi yake Missouri, yeye na Askofu Whitney walianza kurudi Kirtland. Walisafiri kwenye gari la kukokotwa na farasi. Siku moja kitu kiliwatisha farasi na kuwafanya wakimbie kwa kasi. Joseph aliruka kutoka kwenye gari la kukokotwa na farasi, lakini hakuumia. Askofu Whitney aliruka kutoka kwenye gari la kukokotwa na farasi na kuvunja mguu wake. Joseph Smith na Askofu Whitney walikaa katika nyumba ya wageni. Askofu Whitney alipumzika kwa wiki nne. Joseph alikaa pamoja naye wakati mguu wake ukipona. Wakati walipokuwa katika nyumba ya wageni, mtu aliweka sumu kwenye chakula cha Joseph. Akawa mgonjwa sana. Joseph akamwomba Askofu Whitney kumpa baraka. Askofu Whitney alitumia nguvu ya ukuhani kumbariki Joseph, naye akapona. Joseph alimshukuru Mungu kwa kumponya. Wakati Joseph na Askofu Whitney walipokuwa na nafuu ya kutosha kusafiri, walikwenda nyumbani kwa familia zao.