Scripture Stories
Sura ya 29: Ufunuo juu ya Ukuhani: Septemba 1832


Sura ya 29

Ufunuo juu ya Ukuhani

Septemba 1832

Picha
gari la kukokotwa na maksai
Picha
wamisionari wakiondoka kwenye misheni

Wanaume wengi wa Kanisa walienda misheni. Walipofika nyumbani, walikwenda kumwona Joseph Smith huko Kirtland.

Mafundisho na Maagano 84, kichwa cha habari cha sehemu

Picha
Joseph akiwakaribisha wamisionari nyumbani

Wanaume walimwambia Joseph kuhusu misheni zao. Walikuwa wamebatiza watu wengi. Walikuwa na furaha kuhusu misheni zao, na Joseph alikuwa na furaha pia.

Mafundisho na Maagano 84, kichwa cha habari cha sehemu

Picha
Joseph akizungumza na wenye ukuhani

Wamisionari hawa wote walikuwa na ukuhani. Ukuhani ni uwezo wa Mungu. Wamisionari walitaka kujua zaidi juu ya ukuhani.

Picha
nabii Adamu

Yesu alimpa Joseph ufunuo kuhusu ukuhani. Yesu alimwambia kuhusu baadhi ya watu waliokuwa na ukuhani zamani za kale. Adamu, aliyekuwa mtu wa kwanza kuishi duniani, alikuwa na ukuhani.

Picha
Melkizedeki akitoa ukuhani kwa Ibrahimu

Manabii wote wa Agano la Kale walikuwa na ukuhani. Baadhi ya Manabii hawa walikuwa Henoko, Nuhu, Musa, Melkizedeki, na Ibrahimu. Melkizedeki alitoa ukuhani kwa Ibrahimu.

Picha
wenye ukuhani wakitimiza majukumu yao

Yesu alisema kwamba watu lazima wawe na ukuhani ili kuongoza kanisa Lake. Wanaume wenye ukuhani wanaweza kuwabatiza watu na kuwapa kipawa cha Roho Mtakatifu. Wanaweza kubariki sakramenti. Wanaweza kutoa baraka kwa watu walio wagonjwa. Mambo haya yote yanawasaidia Watakatifu wakati wa maisha yao hapa duniani na kuwaandaa kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

Picha
Watakatifu wakiinua mikono kukubali

Yesu alimwambia Joseph kwamba wanaume lazima wawe waadilifu ili kupokea ukuhani. Wale wanaoupokea wanafanya agano, au ahadi, na Mungu. Wanaahidi kuwa waaminifu na kutumia ukuhani ili kuwasaidia watu wengine. Mungu anaahidi kwamba kama wao ni waaminifu, wanaweza kuwa Wanawe maalum. Siku moja Yeye atashiriki pamoja nao vyote Alivyo navyo.

Picha
Wamisionari wakiuhubiria ulimwengu

Yesu alimwambia Joseph Smith kwamba wanaume zaidi wanapaswa kwenda misheni. Wanapaswa kuhubiri injili kwa ulimwengu wote. Wanapaswa kuwafundisha watu kutubu, na wanapaswa kuwabatiza na kuwapa kipawa cha Roho Mtakatifu.

Picha
malaika wakiwasaidia wamisionari

Yesu alisema wamisionari watabarikiwa kama watafanya kazi kwa bidii. Malaika watawasaidia, na Baba wa Mbinguni atawapa kile wanachohitaji.

Picha
Joseph akizungumza na wenye ukuhani

Ufunuo ulimalizika. Joseph na wamisionari walikuwa na furaha ya kujua zaidi kuhusu ukuhani. Walitaka kutumia ukuhani kwa njia iliyo sahihi.

Picha
mwenye ukuhani akitoa baraka

Katika ufunuo wa baadaye, Yesu alimwambia Joseph jinsi wanaume wanavyopaswa kutumia ukuhani. Wanaume hawapaswi kamwe kutumia ukuhani ili kujikweza au kuwa wakatili. Mungu atatoa nguvu ya ukuhani kwa wanaume waadilifu pekee.

Picha
wenye ukuhani wakifanya ibada

Wanaume wanapaswa kutumia ukuhani kwa upendo na ukarimu. Wale wanaomsikiliza Roho Mtakatifu daima watakuwa na nguvu ya ukuhani.

Chapisha