Hadithi za Maandiko
Sura ya 18: Sheria ya Kanisa: Februari 9 1831


Sura ya 18

Sheria ya Kanisa

Februari 9, 1831

ubatizo
Joseph akiandika ufunuo

Katika Kirtland, Ohio, Bwana alitoa ufunuo muhimu sana kwa Joseph Smith. Unaitwa sheria ya Kanisa.

Mafundisho na Maagano 42, kichwa cha habari cha sehemu

mtu akiwa anatawazwa

Bwana alisema Watakatifu wanapaswa kufundisha injili kwa watu wote. Wanaume wanaokwenda misheni wanapaswa kutawazwa kwenye ukuhani na viongozi wa Kanisa.

wamisionari wakifundisha familia

Wamisionari wawili wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja. Wanapaswa kufundisha kutoka kwenye Biblia na Kitabu cha Mormoni. Wanapaswa kuomba ili Roho Mtakatifu awe pamoja nao. Roho Mtakatifu angewaambia cha kufundisha.

wamisionari wakimbatiza mvulana

Wamisionari wanapaswa kuwabatiza watu wanaoiamini injili.

waumini wa Kanisa wakisalimiana

Bwana alisema waumini wa Kanisa wanapaswa kutii Amri Kumi. Hawapaswi kuua. Hawapaswi kusema uongo. Hawapaswi kusema mambo mabaya juu ya watu wengine. Hawapaswi kufanya mambo mengine mabaya.

Watakatifu wakigawiana chakula

Watakatifu wanapaswa kushiriki kile walichonacho na watu wengine. Kushiriki na wengine ni kama kushiriki na Yesu.

Watakatifu wakifanya kazi

Yesu aliwapa Watakatifu amri zingine. Hakuna Mtakatifu anayepaswa kufikiri kuwa yeye ni bora kuliko mtu mwingine. Watakatifu wanapaswa kuwa wasafi. Wanapaswa kufanya kazi kwa bidii.

wazee wakimbariki msichana mgonjwa

Watakatifu wanapaswa kuwahudumia waumini wagonjwa. Wanaume wenye ukuhani wanapaswa kuwabariki wagonjwa. Wale wenye imani wanaweza kuponywa. Hawatakufa kama si wakati wa wao kufa.

roho ya mwanadamu ikiuacha mwili wake

Watakatifu wenye haki hawapaswi kuwa na hofu ya kufa. Kifo ni cha kupendeza kwa watu wenye haki.

Joseph akiwapa maelekezo Watakatifu

Yesu alisema Angefunua mambo mengi kwa waumini wenye haki. Mafunuo haya yangeleta furaha. Bwana aliwaambia Watakatifu kutii sheria ya Kanisa.