Scripture Stories
Utangulizi: Kabla ya Mafundisho na Maagano


Utangulizi

Kabla ya Mafundisho na Maagano

Picha
kijana Joseph akiwa amepiga magoti
Picha
Baba wa Mbinguni akifundisha

Tuliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani. Hatukuwa na miili ya nyama na mifupa kama tulivyo sasa. Tulikuwa roho. Baba yetu wa Mbinguni alitengeneza mpango kwa ajili yetu ili tupokee miili na tuwe zaidi kama Yeye. Huu unaitwa mpango wa wokovu. Mpango huu ulituhitaji tuondoke Kwake kwa muda, na kuja duniani. Kama tunaufuata mpango, tutarudi kuishi pamoja Naye.

Picha
Yesu pamoja na roho zingine

Yesu aliishi na sisi mbinguni. Alitaka kufuata mpango wa Baba wa Mbinguni. Yesu alisema Angekuja duniani ili kufanya iwezekane sisi kurudi mbinguni.

Picha
Baba wa Mbinguni na Shetani

Shetani pia aliishi na sisi mbinguni. Hangefuata mpango wa Baba wa Mbinguni, hivyo Baba wa Mbinguni alimwondoa. Shetani anataka kuharibu mpango wa wokovu.

Picha
nabii wa kale akifundisha

Yesu aliumba dunia ili watoto wa Baba wa Mbinguni waishi. Yesu aliwatuma manabii kuwafundisha watu kuwa wema.

Picha
watu wakiwadhihaki manabii.

Baadhi ya watu waliwatii manabii. Wengine walimtii Shetani na wakawa waovu.

Picha
Nabii wa Agano la Kale anaona ono la yesu

Agano la Kale linaelezea kuhusu watu ambao waliishi kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Manabii waliwafundisha watu hawa kwamba Yesu angekuja duniani ili kuwawezesha kusafishwa kutokana na dhambi na kushinda mauti.

Picha
Nabii wa Kitabu cha Mormoni anaona ono la Kristo

Kitabu cha Mormoni kinaelezea kuhusu watu wengine ambao waliishi zamani za kale. Watu hawa walikuja kutoka Yerusalemu kwenda Amerika. Manabii pia waliwafundisha watu hawa kuhusu Yesu. Aliwatembelea baada ya kufufuka.

Picha
Yesu akiwafundisha wanawake

Agano Jipya linaelezea kuhusu maisha ya Yesu hapa duniani. Linaelezea juu ya kuzaliwa Kwake, mafundisho Yake, na kifo na ufufuo Wake. Yesu aliwafundisha watu injili Yake. Aliwafundisha kutii amri za Baba wa Mbinguni.

Picha
Yesu akiwatawaza Mitume

Yesu aliwachagua watu kumi na wawili kuwa Mitume na akawapa ukuhani. Alianzisha Kanisa Lake. Watu wengi walimpenda Yesu. Walikuwa waadilifu na walitii mafundisho Yake.

Picha
Yesu amesulubishwa msalabani

Shetani hakutaka watu kumfuata Yesu. Aliwajaribu watu kumchukia Yesu, na baadhi yao wakamsulubisha msalabani na kumuua.

Picha
Yesu na Mitume

Siku tatu baada ya Yesu kufa, alifufuka. Alikuwa hai tena! Alizungumza na Mitume Wake na kuwaambia wafundishe injili kwa watu wote. Yesu pia aliwatembelea watu waadilifu katika Amerika. Kisha akaenda mbinguni ili kuwa pamoja na Baba Yake.

Picha
Mitume wakifundisha

Mitume walikuwa viongozi wa Kanisa la Yesu Kristo. Walikwenda katika nchi nyingi na kuwafundisha watu juu ya Yesu. Watu wengi walimwamini Yeye na wakabatizwa. Mitume waliwapa watu waadilifu ukuhani. Kulikuwa na waumini wengi wa Kanisa.

Picha
watu waovu wakiwapiga mawe manabii

Shetani alitaka kuliharibu Kanisa. Aliwajaribu watu kuacha kuamini katika Yesu. Mitume pamoja na waumini wengine wengi wa Kanisa waliuawa. Hatimaye hapakuwa na viongozi wa kuliongoza Kanisa. Baba wa Mbinguni aliondoa ukuhani kutoka duniani.

Picha
kuhani akimbatiza mtoto mchanga

Kanisa ambalo Yesu alianzisha lilitoweka. Watu walianzisha makanisa yao wenyewe. Walibadilisha mafundisho mengi ya Yesu. Pia walibadilisha baadhi ya amri.

Picha
viongozi watatu wa madhehebu tofauti

Mamia ya Miaka ilipita. Kulikuwa na makanisa mengi duniani, lakini hakuna hata moja lililokuwa Kanisa la kweli la Yesu Kristo. Waumini wa makanisa haya waliamini katika Yesu, lakini makanisa hayakuwa na injili ya kweli. Hayakuwa na mamlaka ya ukuhani. Hayakuwa na manabii au mitume.

Picha
mvulana akibatizwa

Yesu alisema kuwa Angerudi tena duniani. Lakini kwanza Kanisa Lake ilibidi lirejeshwe. Ukuhani pia ilibidi urejeshwe. Baraka hizi zilirejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith.

Picha
Nabii Joseph Smith akiandika

Baba wa Mbinguni kwa mara nyingine amewaita manabii na mitume kuongoza Kanisa katika siku yetu. Yesu anatoa ufunuo kwa manabii na mitume ili watuambie kile Anachotaka tujue na kufanya.

Picha
mama akiwasomea familia

Mafundisho na Maagano ni kitabu cha ufunuo kutoka kwa Yesu. Mengi ya ufunuo huu yalitolewa kwa Nabii Joseph Smith. Katika ufunuo huu, Yesu anatoa maelekezo kwa Kanisa Lake na Anafundisha mafundisho ya injili Yake.

Picha
jalada la kitabu hiki

Kitabu unachosoma kinaelezea kuhusu baadhi ya ufunuo katika Mafundisho na Maagano. Pia kinaelezea baadhi ya hadithi kuhusu urejesho na historia ya mwanzo ya Kanisa la Yesu Kristo katika siku za mwisho.

Chapisha