Sura ya 33 Ufunuo kuhusu Yesu Kristo Mei 1833 Katika mojawapo ya mafunuo kwa Nabii Joseph Smith, Yesu alielezea kuhusu Yeye mwenyewe. Alisema watu wanaweza kuuona uso Wake na kumjua Yeye kama watatii amri Zake na kuomba. Mafundisho na Maagano 93:1 Yesu alisema Yeye ni Nuru ya Ulimwengu. Anatuonyesha njia sahihi ya kuishi. Mafundisho na Maagano 93:2 Yesu aliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya dunia kutengenezwa. Yesu aliumba dunia na vitu vyote vilivyo ndani yake. Mafundisho na Maagano 93:7–10 Yesu hakuwa kama Baba yake wa Mbinguni mwanzoni. Hakujua mambo yote ambayo Baba Yake alijua, na hakuwa na nguvu zote na utukufu ambao Baba Yake alikuwa nao. Yesu alijaribu sana kuwa kama Baba Yake. Hatua kwa hatua Yeye alipokea nguvu na utukufu wa Baba Yake. Mafundisho na Maagano 93:12–17 Yesu alisema tunapaswa kutii amri za Mungu. Kadiri tunavyotii, tunaweza kuja kujua mambo yote. Tunaweza pia kuwa kama Mungu na kupokea utimilifu wa baraka Zake. Mafundisho na Maagano 93:20, 27–28 Yesu alisema Shetani hataki watu wajue ukweli na kuwa kama Mungu. Yesu alimwambia Joseph aifundishe familia yake ukweli. Mafundisho na Maagano 93:39–40, 48 Yesu pia alimwambia Frederick G. Williams na Sidney Rigdon kufundisha familia zao kuhusu ukweli na kutii amri. Hapo Shetani asingeweza kuwa na nguvu juu yao. Mafundisho na Maagano 93:41–44