Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136: “Yeye ‘Ametia Muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe’”


“Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136: ‘Yeye “Ametia muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe,”’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 22–28. Mafundisho na Maagano 135–136,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
mwonekano wa nje wa Gereza la Carthage

Gereza la Carthage

Novemba 22–28

Mafundisho na Maagano135–136

Yeye “Ametia Muhuri Huduma Yake na Kazi Yake kwa Damu Yake Mwenyewe”

Unapojiandaa kufundisha Mafundisho na Maagano 135–36, tafuta kanuni ambazo zimekuvutia maishani mwako. Fikiria jinsi mawazo katika muhtasari huu yanavyoweza kuwasaidia watoto kujifunza na kuzitumia kanuni hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuelezea kitu wanachokumbuka kujifunza mwaka huu kuhusu Joseph Smith na kile alichokamilisha. Onesha picha kutoka kwenye Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia ya mwaka huu au kutoka kurasa zilizopita za shughuli ili kuwasaidia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 135:1–2

Joseph Smith na Hyrum Smith walitoa maisha yao kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.

Hadithi ya kifo cha kishahidi ya Joseph na Hyrum Smith inaweza kuwasaidia watoto kuwa na shukrani kwa shuhuda na dhabihu za watu hawa maarufu.

Shughuli Yamkini

  • Tumia “Sura ya 57: Nabii Ameuawa” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 201–5) ili kuwaambia watoto kuhusu jinsi Nabii Joseph Smith na kaka yake Hyrum walivyokufa. Au acha mmoja wa watoto asimulie hadithi hiyo. Toa ushuhuda wako kwamba Joseph Smith alikuwa nabii wa kweli na kwamba alitoa uhai wake kwa ajili ya Bwana na injili Yake.

  • Shiriki na watoto vifungu vichache vya maneno kutoka kwenye mstari wa Kitabu cha Mormoni ambao Hyrum Smith aliusoma kabla ya kwenda Gereza la Carthage, ulioandikwa katika Mafundisho na Maagano 135:5. Zungumza kuhusu jinsi mstari huu ulivyomfariji Hyrum. Shiriki maandiko ambayo hukupa wewe faraja wakati ukiwa na hofu au huzuni.

Mafundisho na Maagano135:3

Joseph Smith ni Nabii wa Mungu.

Kwa mwaka mzima, watoto wamejifunza yale Bwana aliyoyafunua kupitia Nabii Joseph Smith. Unaweza kuwasaidia kukumbuka na kushukuru jinsi kazi ya Joseph inavyobariki maisha yao.

Shughuli Yamkini

  • Onesha vitu ambavyo huwakilisha kazi za Nabii Joseph Smith, kama vile Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, au picha ya wamisionari au hekalu. Kwa kutumia vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 135:3, shiriki na watoto baadhi ya vitu ambavyo Bwana alifanya kupitia Joseph Smith kwa ajili ya wokovu wetu. Waalike watoto kuchagua moja ya vitu hivi na kuwaelezea wengine kwa nini wanashukuru kwa ajili ya hicho kitu.

  • Watoto wanapopaka rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, imba au piga nyimbo kuhusu Joseph Smith, kama vile “Praise to the Man” (Nyimbo za Kanisa, na. 27). Shiriki hisia zako kuhusu Nabii.

    Picha
    Joseph Smith

    Nabii wa Amerika, na Del Parson

Mafundisho na Maagano 136

Mungu hutupatia sisi amri ili kutusaidia.

Watakatifu walikabiliwa na majaribu mengi katika miaka iliyofuatia kifo cha Joseph Smith. Je, ushauri uliotolewa na Bwana kwa Watakatifu unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Shiriki na watoto baadhi ya changamoto Watakatifu walizokabiliana nazo wakati wakiondoka Nauvoo na kukusanyika katika Winter Quarters (ona sura ya 60 na 62 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 211–16, 222–24). Weka picha ya Hekalu la Nauvoo upande mmoja wa chumba, na tengeneza kibanda rahisi cha makazi upande mwingine—pengine kwa kutumia blanketi na baadhi ya viti au meza. Waalike watoto kukusanyika jirani na picha hiyo, na waambie kwamba mwaka mmoja na nusu baada ya kufa kwa Joseph Smith, Watakatifu walilazimishwa kuondoka Nauvoo. Waalike watoto kuondoka kutoka kwenye hilo hekalu na kukusanyika katika kibanda kuashiria safari kuelekea Winter Quarters.

  • Elezea kwamba Bwana alitoa ufunuo kwa Brigham Young, unaopatikana katika Mafundisho na Maagano 136, ili kuwasaidia Watakatifu wakati wakisafiri kwenda Bonde la Salt Lake. Soma vifungu vichache vya maneno kutoka sehemu ya 136 vyenye ushauri ambao watoto wadogo wanaweza kuelewa, na waalike kuigiza au wachore kile Bwana alichowaomba Watakatifu kufanya wakiwa wanasafiri. Kwa mfano, watoto wangeweza kujichora wao wenyewe wakiwa wanarudisha kitu walichokiazima kutoka kwa rafiki, au wangeweza kuimba wimbo wa Msingi wakati wakicheza kuzunguka moto bandia wa kambi (ona mstari wa 25, 28).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 135

Joseph Smith na Hyrum Smith walitoa maisha yao kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.

Kusikia kuhusu dhabihu ya Joseph Smith na Hyrum Smith kunaweza kuimarisha imani ya watoto na hamu yao ya kuwa wakweli katika shuhuda zao.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto washiriki na wengine kile wanachokijua kuhusu jinsi Joseph na Hyrum Smith walivyouawa. Kama wanahitaji msaada, warejeshe kwenye Mafundisho na Maagano 135:1 au “sura ya 57: Nabii Ameuawa” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 201–5). Waalike watoto kufikiria kuwa walikuwa wakiishi Nauvoo wakati Nabii anakufa. Waombe washiriki na wengine jinsi ambavyo wangejisikia. Toa ushuhuda wako juu ya Joseph Smith, na waalike watoto nao kufanya vivyo hivyo.

  • Onesha picha za manabii (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 14, 1867). Je, ni baadhi ya mambo gani Mungu amewaomba manabii kufanya? Elezea kwamba Bwana anaahidi baraka kwa manabii Wake kwa ajili ya dhabihu wanazofanya katika huduma Yake (ona Mathayo 10:39).

Mafundisho na Maagano135:3

Joseph Smith ni Nabii wa Mungu.

Kama manabii wote, Joseph Smith alishuhudia juu ya Yesu Kristo na alitufundisha jinsi ya kuja Kwake. Wasaidie watoto waone jinsi Joseph Smith alivyokamilisha huduma yake.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 135:3, na waombe watoto watambue yale Joseph Smith aliyokamilisha. Andika ubaoni kile walichokipata. Waalike watoto kuchagua moja ya vitu hivi na kuwaelezea wengine kwa nini wanashukuru kwa ajili ya hicho kitu.

  • Wahimize watoto kila mmoja kumfikiria rafiki au mpendwa ambaye hajui mengi kuhusu Joseph Smith. Wangesema nini kama mtu huyo angeuliza, “Je, ni kwa nini Joseph Smith ni muhimu sana kwako?” Waalike watoto kufanya mazoezi ya kile ambacho wangesema kwa mtu huyu.

Mafundisho na Maagano 136:4, 10–11, 18–30

Bwana anaweza kunibariki ninapokuwa nahangaika.

Baada ya Joseph Smith kuuawa, Watakatifu walifukuzwa kutoka Nauvoo. Brigham Young aliwaongoza kwenda Winter Quarters, mahali walipojiandaa kwa safari ndefu kwenda Bonde la Salt Lake.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwa kifupi uzoefu wa Watakatifu baada ya Nabii Joseph Smith kuuawa (ona sura ya 5860, na 62 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, kurasa 206–8, 211–16, 222–24). Waalike watoto kufikiria jinsi ambavyo wangejisikia kama wangetakiwa kuziacha nyumba zao na kutafuta mahali pengine pa kuishi nyikani. Elezea kwamba katika Mafundisho na Maagano 136, Bwana alitoa ushauri ili kuwasaidia Watakatifu katika safari yao. Mpangie kila mtoto mistari michache kutoka katika ufunuo huu, kama vile mstari wa 4, 10–11, 18–30, na waombe watoto kila mmoja atafute kitu ambacho kingeweza kuwasaidia kuondokana na wasiwasi na hofu zao.

  • Wasaidie watoto kufikiria majaribu watu wanayokabiliana nayo leo. Waalike watafute kitu katika sehemu ya 136 ambacho wanaweza kushiriki na wengine ili kumtia moyo mtu ambaye anapitia katika wakati mgumu. Watoto wanaweza pia kupata ujumbe unaowatia moyo katika “Come, Come, Ye Saints” (Nyimbo za Kanisa, na. 30), wimbo ambao Watakatifu waliimba katika safari yao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao au rafiki kwa nini wana shukrani kwa Nabii Joseph Smith.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto ni wachangamfu. Wakati mwingine unaweza kuhisi kwamba uchangamfu wa watoto ni vurugu kwenye kujifunza. Lakini unaweza kujenga juu ya asili yao ya uchangamfu kwa kuwaalika kuchora, kuimba, au kuigiza kanuni ya injili (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26).

Chapisha