Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 1–7. Mafundisho na Maagano 125–128: “Sauti ya Furaha kwa Walio Hai na Wafu”


“Novemba 1–7. Mafundisho na Maagano 125–128 : ‘Sauti ya Furaha kwa Walio Hai na Wafu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 1–7. Mafundisho na Maagano 125–128,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
familia pamoja na mababu katika ulimwengu wa roho

Sisi pamoja na Wao na Wao pamoja na Sisi, na Caitlin Connolly

Novemba 1–7

Mafundisho na Maagano 125–128

“Sauti ya Furaha kwa Walio Hai na Wafu”

Ikiwa unafundisha watoto wadogo na unahitaji msaada wa ziada, ona “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa nyenzo hii.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wasaidie watoto kufikiria kitu walichojifunza wiki hii nyumbani au katika darasa la Msingi. Wape dakika chache ili wachore picha ya kile walichofikiria na wakishiriki kwa darasa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 126:3

Mimi naipenda familia yangu.

Baada ya Brigham Young kurejea nyumbani kutoka kuhubiri injili, Bwana alimwambia afokasi katika kuitunza familia yake.

Shughuli Yamkini

  • Waelezee watoto habari kuhusu Brigham Young iliyoko katika “Sura ya 50: Watakatifu huko Nauvoo” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 184), au eleza kwa kifupi Mafundisho na Maagano 126 katika maneno yako mwenyewe. Kisha soma Mafundisho na Maagano 126:3 kwa watoto, ukisisitiza kifungu cha maneno “kuishughulikia vizuri familia yako.” Inamaanisha nini kushughulikia familia zetu? Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kuonesha upendo kwa wanafamilia wao.

  • Kabla ya darasa, waalike watoto kuleta picha ya familia zao (au waombe wachore picha). Kisha waombe kushiriki kitu wanachopenda kuhusu familia zao. Onesha picha ya familia yako, nao wafanye vivyo hivyo. Eleza ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tuwajali wanafamilia wetu. Imbeni wimbo unaofundisha ukweli huu, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198).

Mafundisho na Maagano 128:5, 12

Watoto wote wa Mungu wanahitaji nafasi ya kubatizwa.

Katika kuongezea kwenye kuwasaidia watoto kujiandaa kufanya maagano yao ya ubatizo, wafundishe kwamba tunaweza kuwasaidia wale waliokufa pasipo ubatizo kupokea baraka hizo.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Yesu Kristo akiwa anabatizwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 35), au onesha video ya “The Baptism of Jesus” (ChurchofJesusChrist.org). Waulize watoto kama wamewahi kuona mtu anabatizwa. Je wanakumbuka nini kuhusu hilo? Tumia picha au video kuwaonesha watoto kwamba wakati tunapobatizwa, tunazama kabisa chini ya maji na kisha tunainuka tena, kama vile Yesu alivyofanya. Fungua Mafundisho na Maagano 128:12, na ueleze kwamba Joseph Smith alifundisha kwamba kubatizwa kunatukumbusha juu ya Ufufuko.

  • Waambie watoto kuhusu mtu fulani unayemjua (kama vile babu au bibi) aliyefariki dunia pasipo kubatizwa. Soma Mafundisho na Maagano 128:5, na acha wapeane zamu kushika picha ya kisima cha ubatizo cha hekaluni (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anaruhusu sisi tubatizwe hapa duniani kwa niaba ya watu waliokufa. Kwa njia hii watoto wote wa Mungu wanaweza kubatizwa na kufanya maagano na Yeye.

Mafundisho na Maagano 128:18

Baba wa Mbinguni anataka mimi nijifunze kuhusu historia ya familia yangu.

Kuna njia nyingi rahisi ambazo kwazo watoto wadogo wanaweza kushiriki katika kazi ya historia ya familia. Wasaidie kuhisi upendo kwa ajili ya watu katika mti wao wa familia.

Shughuli Yamkini

  • Tengeneza mnyororo wa karatasi wenye majina ya watu wa familia yako (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii), na ulete ili kuwaonesha darasa. Simulia mambo machache kuhusu watu kwenye mnyororo wako. Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 128:18, na eleza kwamba Joseph Smith alifundisha kwamba “kuna muunganiko … kati ya mababu na watoto.” Wasaidie watoto kutengeneza minyororo ya familia zao, na waalike wapeleke minyororo yao nyumbani kwao na wazazi wao wawasaidie kuongeza majina ya mababu zao.

  • Waombe watoto kusimulia kitu kuhusu mmoja wa babu au bibi zao. Simulia moja ya hadithi zako uzipendazo kuhusu wazazi wako au mababu zako. Onesha picha ikiwezekana. Wahimize watoto kujifunza zaidi kuhusu mababu zao na wahenga wengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 126

Naweza kusaidia kuitunza familia yangu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuwatumikia wanafamilia wao katika njia bora zaidi?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 126:3. Kwa nini unafikiri Baba wa Mbinguni alikuwa amemwomba Bringham Young “kuishughulika vizuri familia [yake]”? Je, ni kwa namna gani sisi tunaweza kufanya vivyo hivyo kwa familia zetu? Tengeneza orodha ya mambo tunayoweza kufanya sasa ili kuhudumia familia zetu. Je, ni kwa namna gani kufanya mambo haya kutatusaidia kuwa zaidi kama Baba yetu wa Mbinguni?

  • Shiriki na watoto hadithi ya Dada Carole M. Stephens kuhusu mjukuu wake Porter (ona “Tunayo Sababu Kubwa ya Kufurahi,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 115). Je, Porter alifanya nini ili kuitunza familia yake? Je, sisi tunawezaje kuiga mfano wake?

Mafundisho na Maagano 128:1, 15–18.

Ubatizo kwa niaba ya wafu hutengeneza “muunganiko” kati yangu mimi na mababu zangu.

Joseph Smith alifundisha kwamba ubatizo kwa niaba ya wafu hutuunga sisi na mababu zetu kama vile viungo katika mnyororo. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuhisi furaha inayokuja kutokana na kujifunza kuhusu mababu zetu na kuhakikisha kwamba kazi za hekaluni zinafanyika kwa niaba yao?

Shughuli Yamkini

  • Ligawe darasa katika makundi mawili, na litake kundi la kwanza lisome Mafundisho na Maagano 128:1 ili kupata somo ambalo lilijaa katika mawazo ya Joseph Smith. Liombe kundi jingine kusoma mstari wa 17 na kutafuta ni somo lipi alilolifikiria kuwa “tukufu zaidi.” Waache waelezee kile walichopata, na kuzungumza kuhusu kwa nini somo hili ni tukufu zaidi. Kama inawezekana, mwalike kijana ambaye amewahi kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu asimulie uzoefu wake na aeleze kwa nini tunafanya kazi hii.

  • Zingatia kutumia somo la vitendo ili kuonesha kwamba tunahitaji kuwasaidia mababu zetu ambao hawakubatizwa. Kwa mfano, onesha zawadi, lakini iweke mahali pasipofikiwa na mmoja wa watoto. Mwambie mtoto huyo kwamba anaweza kuchukua zawadi hiyo lakini asitoke kwenye kiti chake. Waulize watoto wengine kile wanachoweza kufanya ili kumsaidia mtoto huyo kupata zawadi yake. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 128:15, na zungumza kuhusu jinsi inavyohusiana na somo la vitendo.

  • Waalike watoto kutengeneza mnyororo wa karatasi wenye majina ya wazazi wao, babu na bibi, babu na bibi wakuu, na kadhalika (ona ukurasa wa shughuli kwa ajili ya somo hili). Kama watoto hawajui majina ya mababu zao, watie moyo kutafuta majina hayo na kuyaandika kwenye mnyororo huo wakiwa nyumbani. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 128:18 ili kujua “muunganiko” ni kitu gani ambacho hufanya historia ya familia yetu iwe “nzima na kamilifu.” Simulia hadithi kuhusu babu ambayo inakusaidia wewe kuhisi umeunganishwa naye. Au onesha video “Courage: I think I Get It from Him” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Waoneshe watoto kibali cha hekaluni, na waambie jinsi ulivyokipata. Wasaidie kutazamia kwa hamu kupata kibali chao wenyewe cha kuingia hekaluni ili waweze kwenda hekaluni na kubatizwa kwa niaba ya mababu zao.

    Picha
    mvulana akiwa na kadi za majina ya familia

    Tunaweza kutafuta majina ya mababu zetu na kufanya ibada za hekaluni kwa niaba yao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumwomba mtu nyumbani ili awasaidie kujifunza zaidi kuhusu historia ya familia zao. Wanaweza kuomba kusikiliza hadithi juu ya babu fulani au kutumia FamilySearch.org ili kupata majina ya mababu ambao hawajabatizwa.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kuelezea ubunifu wao. Watoto wanapojenga, kuchora, au kupaka rangi kitu kinachohusiana na hadithi au kanuni wanayojifunza, mara nyingi wanaikumbuka vizuri zaidi. Wanaweza pia kutumia kile walichobuni ili kuwafundisha wengine. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25.)

Chapisha