Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132: “Kama Tunapata Baraka Yoyote Ile kutoka kwa Mungu, Ni Kutokana na Utii”


“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132: ‘Kama Tunapata Baraka Yoyote Ile kutoka kwa Mungu, Ni Kutokana na Utii,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 8–14. Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Joseph Smith Akifundisha katika Nauvoo

Joseph Smith akiwa Nauvoo, 1840, na Theodore Gorka

Novemba 8–14

Mafundisho na Maagano 129–132

“Kama Tunapata Baraka Yoyote Ile kutoka kwa Mungu, Ni kutokana na Utii”

Mzee David A. Bednar alieleza: “Kuzungumzia na kusimulia pekee siyo kufundisha. Kuhubiri injili katika njia ya Bwana kunajumuisha kuchunguza na kusikiliza na kutambua” (“Becoming a Preach My Gospel Missionary,” New Era, Okt. 2013, 6). Je, Roho anakufundisha nini unapochunguza na kusikiliza kutoka kwa watoto unaowafundisha?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Teua mada kutoka sehemu ya 129–32, na acha watoto wakuambie kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu mada hiyo. Kwa mfano, wao wanajua nini kuhusu Baba wa Mbinguni au Uungu? Kuhusu ndoa ya milele? Kuhusu ufalme wa selestia?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 130:20–21; 132:5

Baraka huja kutokana na utii kwa Mungu.

Joseph Smith alifundisha kwamba kila baraka kutoka kwa Mungu msingi wake ni utiifu wetu kwa amri Zake. Ni kwa jinsi gani unaweza kufundisha kanuni hii katika njia ambayo watoto wataelewa?

Shughuli Yamkini

  • Elezea mfanano rahisi kwa watoto ambao unaonesha jinsi gani ilivyo muhimu kufuata maelekezo; kwa mfano, zungumza nao kuhusu hatua tunazolazimika kuchukua ili kuandaa chakula au kucheza mchezo au kujenga kitu fulani. Je, ni kitu gani hutokea wakati tunapokuwa hatufuati maelekezo? (Labda una uzoefu binafsi unaoweza kuushiriki.) Soma Mafundisho na Maagano 130:21, na linganisha maelekezo haya na amri ambazo ni lazima tuzifuate ili kupokea baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

  • Waulize watoto kama wanaweza kufikiri juu ya wakati ambapo walitii moja ya amri za Mungu. Je, walijisikiaje? Imbeni pamoja wimbo kuhusu utii, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47), na zitambueni baraka za utii zilizotajwa katika wimbo huu. Jadili baadhi ya mambo ambayo Mungu ametuamuru sisi tufanye. Je, ni kwa namna gani Mungu anatubariki sisi wakati tunaposhika amri?

Mafundisho na Maagano 130:22

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wana miili isiyokufa ya nyama na mifupa.

Tunapoelewa kwamba Mungu Baba na Yesu Kristo wanayo miili kama yetu sisi, tunahisi kuwa karibu zaidi na Wao, na uhusiano wetu na Wao unaimarika.

Shughuli Yamkini

  • Waoneshe watoto picha ya Yesu Kristo, na waalike watoto kuonesha kwa kidole macho Yake, mdomo, na viungo vingine vya mwili Wake. Kisha waalike kusimama na kuonesha kwa kidole viungo hivyo vya miili yao wenyewe. Soma kutoka Mafundisho na Maagano 130:22: “Baba anao mwili wa nyama na mifupa … ; na Mwana vile vile.” Toa ushuhuda kwamba miili yetu ni kama ile ya Baba wa Mbinguni na Yesu.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu miili yetu, kama vile “Head, Shoulders, Knees, and Toes” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 275), na waalike watoto kufanya matendo yanayoendana na maneno. Waombe watoto wakutajie baadhi ya mambo wanayoweza kufanya kwa kutumia miili yao. Elezea shukrani yako kwa ajili ya mwili ambao Mungu amekupatia. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha kwamba tunashukuru kwa zawadi hii maalumu?

  • Waalike watoto kuchora picha za Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, na wao wenyewe. Wasaidie kuona namna ambavyo miili yetu ni kama miili ile ya Baba wa Mbinguni na Yesu.

Mafundisho na Maagano 132:19

Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja milele.

Kupitia uwezo wa kuunganisha wa Bwana na ibada za hekaluni, mahusiano yetu ya familia yanaweza kudumu milele kama tutashika maagano yetu.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya mifano ya vitu ambavyo havidumu milele—chakula ambacho huharibika, maua ambayo hunyauka, na vinginevyo. Onesha picha ya familia yako, na elezea jinsi unavyojisikia kuhusu wao. Toa ushuhuda kwamba Bwana amefanya iwezekane, kupitia ibada za hekaluni, kwa familia kudumu milele.

  • Fungua Mafundisho na Maagano kwenye sehemu ya 132, na waambie watoto kwamba huu ni ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith kuhusu ndoa na familia. Waoneshe mstari wa 19, na onesha kwenye maneno “milele yote” unapoyasoma. Waalike watoto kusoma maneno haya pamoja na wewe.

  • Wasaidie watoto kutengeneza wanasesere wa karatasi wakiwakilisha wanafamilia wao (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Kata wanasesere hao, na waweke pamoja ndani ya bahasha au wabane pamoja kwa pini ya kubania karatasi ili kuwakilisha uwezo wa kuunganisha ambao unaweza kufanya familia zetu kuwa za milele.

    Picha
    mwanamke na msichana mdogo wakiwa kwenye viwanja vya hekalu

    Ibada za hekaluni huruhusu familia kuwa pamoja milele.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 130:18–19

Baba wa Mbinguni anataka nipate maarifa na akili.

Vitu vingi tunavyopata katika maisha haya havitakwenda pamoja na sisi katika maisha yajayo. Lakini “maarifa na akili” zetu zitakwenda nasi (Mafundisho na Maagano 130:19).

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kushiriki nawe kitu wanachojifunza shuleni au kutoka kwa wazazi wao. Waalike kusoma Mafundisho na Maagano 130:18–19 ili kujua kile kitakachotokea kwenye maarifa na akili zetu katika maisha yajayo.

  • Je, mstari wa 19 hufundisha nini kuhusu jinsi tunavyopata maarifa na akili? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa wenye bidii na watiifu wakati tunapotafuta kujifunza? (Kwa ziada katika mada hii, ona “Elimu” katika Kwa Nguvu ya Vijana [kurasa 9–10].)

Mafundisho na Maagano 130:20–21; 132:5, 21–23

Baraka huja kutokana na utii kwa Mungu.

Tafakari jinsi Bwana anavyokubariki wakati unapotii sheria Zake. Je, ni matukio gani ungeweza kushiriki na watoto ili kuwatia moyo?

Shughuli Yamkini

  • Imbeni wimbo kuhusu utii, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47), na waalike watoto kusoma Mafundisho na Maagano 130:20–21 na 132:5. Wasaidie watoto kutafuta maneno na mawazo katika maandiko ambayo ni sawa na yale yaliyomo katika wimbo. Ni kwa jinsi gani sisi tunapokea baraka kutoka kwa Mungu? Waombe watoto kushiriki jinsi walivyobarikiwa kwa sababu ya kutii sheria za Mungu.

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 132: 21–23, na waalike watoto kuchora picha zenye kuwakilisha kile wanachojifunza kutoka kwenye mistari hii. Watie moyo wa kuwa wabunifu, na pendekeza kwamba wajumuishe katika michoro yao sheria au amri ambazo hutusaidia sisi kubaki kwenye njia nyembamba iendayo kwenye uzima wa milele.

Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:15, 19

Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja milele.

Bila kujali hali ya sasa ya familia zetu, tunaweza kufanya chaguzi zetu sasa ambazo zitatuandaa ili kupokea baraka za familia ya milele katika siku za usoni.

Shughuli Yamkini

  • Waombe baadhi ya watoto kusoma Mafundisho na Maagano 131:1–4 na wengine kusoma 132:15. Wasaidie kugundua mistari hii inafundisha nini kuhusu ndoa. Chagua vifungu vya maneno muhimu kutoka 132:19 (kama vile “kama mtu ataoa mke,” “agano lisilo na mwisho,” “kuunganishwa,” “kukaa katika agano langu,” “milele yote,” na “milele na milele”), na waombe watoto kutafuta vifungu hivi vya maneno katika mstari huu. Je, vifungu hivi vya maneno vinatufundisha nini sisi kuhusu ndoa?

  • Imbeni “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188), au rejelea “Sura ya 55: Ufunuo kuhusu Ndoa” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 198). Waombe watoto kusikiliza na kujiandaa kuelezea kile tunacholazimika kufanya ili familia zetu zipate kuwa za milele. Toa ushuhuda wako kuwa bila kujali hali za sasa za familia zetu, tunaweza kujiandaa sisi wenyewe kuwa sehemu ya familia ya milele.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuziambia familia zao jinsi wanavyowapenda na wanataka kuungana nao kama familia milele.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa makini kwa hali za familia. “Watoto leo wanajikuta katika hali nyingi tofauti za kifamilia na zenye mipangilio changamani. … [Sisi] tunahitaji kuwafikia [wale] wenye kujiona wapweke, wameachwa nyuma, au nje ya ua” (Neil L. Andersen, “Yeyote Awapokeaye, Anipokea Mimi,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 49, 52).

Chapisha