Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138: “Hakuna Silaha Iliyotengenezwa dhidi Yenu Itakayofanikiwa”


“Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138: ‘Hakuna Silaha Iliyotengenezwa Dhidi Yenu Itakayofanikiwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Novemba 29–Desemba 5. Mafundisho na Maagano 137–138,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

watu katika ulimwengu wa roho

Joseph anamwona baba yake, mama yake, na kaka yake katika ufalme wa selestia (Joseph Smith’s Vision of the Celestial Kingdom, Robert Barrett).

Novemba 29–Desemba 5

Mafundisho na Maagano 137–138

“Ono la Ukombozi wa Wafu”

Tafuta kanuni katika mafunuo haya ambazo zinaonekana kuwa muhimu kwa watoto unaowafundisha. Je, ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia kuelewa kanuni hizi?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha ya Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho, kama vile moja iliyoko katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu ulimwengu wa roho.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 137:1–5

Mungu amenipa njia ya mimi kuwa pamoja na familia yangu milele.

Katika Ono, Joseph Smith aliwaona wanafamila yake wakiwa pamoja katika ufalme wa selestia. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kutumia ono lake kuwafundisha watoto kwamba familia zinaweza kuwa pamoja milele?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya mtu katika familia yako, na zungumza ni jinsi gani wewe unataka kuwa pamoja naye katika ufalme wa selestia. Elezea kwamba Alvin kaka wa Joseph Smith alikufa akiwa kijana mdogo na Joseph alimkumbuka sana. Soma Mafundisho na Maagano 137:1, 5, na waulize watoto Joseph Smith alimwona nani katika ono lake la ufalme wa selestia (ona pia Hadithi za Mafundisho na Maagano, 152–53). Waalike watoto kunyoosha mikono yao kwa upana ili kuonesha ni jinsi gani wanazipenda familia zao, na waombe waeleze ni kwa nini wao wanapenda kuwa pamoja na familia zao katika ufame wa selestia.

  • Tumia Mafundisho na Maagano 137:1–5 na ukurasa wa shughuli ya wiki hii ili kuwasaidia watoto kugundua maelezo ya kina kuhusu ono la Joseph Smith la ufalme wa selestia. Waalike kuchora picha za wao wenyewe pamoja na familia zao kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii wakati wewe ukipiga au kuimba wimbo kuhusu familia, kama vile “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188).

Mafundisho naa Maagano 138:6–11

Roho Mtakatifu anaweza kunisaidia kuelewa maandiko.

Maandiko yanaweza wakati mwingine kuwa magumu kueleweka, hususani kwa watoto. Mafundisho na Maagano 138:11 inafundisha kwamba Roho Mtakatifu anaweza kufungua “macho ya ufahamu [wetu].”

mvulana akisoma maandiko

Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kuelewa kile tunachosoma katika maandiko.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Rais Joseph F. Smith (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 127). Eleza kwamba yeye alikuwa Rais wa sita wa Kanisa, na siku moja alikuwa akisoma maandiko na kuyatafakari (akifikiria kuhusu kile yanachomaanisha). Unaposoma Mafundisho na Maagano 138:6, 11, waalike watoto kujifanya wao ni Rais Smith na wafanye matendo yanayoendana na maneno.

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambapo wewe ulitafakari kitu katika maandiko na Roho Mtakatifu akakusaidia kukielewa kitu hicho. Imbeni pamoja wimbo kuhusu kujifunza maandiko, kama vile “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109). Je, wimbo huu unasema tunapaswa kufanya nini ili kuelewa maandiko?

Mafundisho na Maagano 138:18–35

Watoto wote wa Baba wa Mbinguni watapata nafasi ya kusikia injili.

Baada ya Yesu Kristo kusulubiwa, Aliwatembelewa Watakatifu Wake waaminifu katika ulimwengu wa roho. Aliwaamuru kufundisha injili kwa wale ambao hawakuwa wameipokea.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya kaburi (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 58, 59 au Picha za Biblia, na. 14), au chora picha ya kaburi ubaoni. Onesha picha ya Mwokozi katika ulimwengu wa roho wakati mwili wake ukiwa kaburini, (kama ile iliyoko kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Unapofanya hivyo, waulize maswali ili kuwasaidia watoto kutambua maelezo muhimu katika Mafundisho na Maagano 138:18–19, 23–24, 27–30, kama vile Yesu aliwatembelea nani, walihisi namna gani, na aliwaambia wafanye nini.

  • Onesha picha ya wamisionari (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 109, 110), na waombe watoto kuelezea kile wamisionari wanachofanya. Unaweza pia kuwaalika kuigiza baadhi ya mambo wanayofanya wamisionari. Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 138:31–34 . Elezea kwamba kama vile wamisionari walivyo hapa duniani, kuna wamisionari pia katika ulimwengu wa roho ambao huwafundisha watu huko.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 137:1–5

Mungu amenipa njia ya mimi kuwa pamoja na familia yangu milele.

Joseph Smith alipata ono la ufalme wa selestia na akawaona wazazi wake na kaka yake Alvin huko. Ono hili linatufundisha kwamba kama sisi ni waadilifu, mahusiano yetu ya kifamilia yanaweza kuendelea katika maisha yajayo.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Mafundisho na Maagano 137:1–5 na kuchora picha ya kile wanachosoma (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Je, ni kwa jinsi gani Joseph Smith alijisikia wakati alipowaona wanafamilia yake katika ufalme wa selestia?

  • Onesha video ya “Families Can Be Together Forever” (ChurchofJesusChrist.org), au imbeni wimbo kuhusu familia, kama vile “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188). Je, video au wimbo vinatufundisha nini kuhusu kile tunachoweza kufanya ili kufanya familia zetu kuwa za milele?

Mafundisho na Maagano 138:1–11

Ninapotafakari maandiko, Roho Mtakatifu anaweza kunisaidia kuyaelewa.

Je, watoto wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Rais Joseph F. Smith ambacho kinaweza kuboresha namna wanavyojifunza maandiko?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kusoma Mafundisho na Maagano 138:1–11, na wasaidie kuandika kwa ufupisho sentensi-moja ya tukio la Rais Joseph F. Smith. Je, yeye alifanya nini ambacho kiliongoza kwenye ono hili la ajabu? Je, inamaanisha nini kutafakari au kuwaza juu ya maandiko?

  • Waulize watoto kile wanachofanya wanapokuwa na maswali kuhusu injili. Shiriki baadhi ya mifano kutoka kwenye maandiko au ya maisha yako mwenyewe ya wakati kutafakari maandiko kulivyoleta uelewa kutoka kwa Roho (ona, kwa mfano, 1 Nefi 11:1–6; Mafundisho na Maagano 76:19–24; Joseph Smith—Historia ya 1:11–12).

Mafundisho na Maagano 138:12–35

Watoto wote wa Baba wa Mbinguni watapata nafasi ya kusikia injili.

Rais Joseph F. Smith alijifunza kwamba kazi ya kuhubiri injili inaendelea katika ulimwengu wa roho. Kazi hii inahakikisha kwamba kila mmoja atakuwa na nafasi ya kuikubali injili.

Shughuli Yamkini

  • Ubaoni, orodhesha baadhi ya mistari kutoka sehemu ya 138. Kisha orodhesha, katika utaratibu tofauti, maelezo yanayofanya muhtasari wa kila mstari Waalike watoto kulinganisha maelezo na mstari sahihi. Mistari ingeweza kujumuisha 12–16 (roho waadilifu wanakusanyika kumsubiri Yesu awatokee), 18–19 (Mwokozi anawatokea roho walio waadilifu), 29–30 (Yesu anawateua wajumbe kuhubiri injili), 31–35 (roho waadilifu wanahubiri injili), na kadhalika. Baada ya watoto kufanya ulinganisho, waulize wamejifunza nini kutoka kwenye mistari hii.

  • Waombe baadhi ya watoto kusoma Mafundisho na Maagano 138:33 ili kutafuta ni kanuni gani za injili zilifundishwa kwa roho za wafu. Waombe watoto wengine kusoma kanuni zinazofundishwa katika Makala ya Imani 1:4. Je, nini kinafanana katika mistari hii, na nini ni tofauti? Je, hii inatufundisha nini kuhusu Baba wa Mbinguni na mpango Wake?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kupanga muda wiki hii wakati watakapotafakari maandiko wanayosoma.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba kimya kimya au kwa mvumo wimbo wa Msingi au kuonesha picha ya Yesu.