Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2: “Tunaamini”


“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2: ‘Tunaamini,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Desemba 6–12. Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

mfarishi ukionesha mikono ya ngozi za rangi nyingi

Kwa Wanaume Wote Wenye Kustahili, na Emma Allebes

Desemba 6–12

Makala ya Imani na Matamko Rasmi 1 na 2

“Tunaamini”

Unaposoma wiki hii na kutengeneza mpango wa kufundisha, fikiria namna unavyoweza kuwasaidia watoto katika darasa lako kuimarisha imani yao katika kweli za msingi za injili.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Rusha mpira kwa mtoto, na muombe mtoto kushiriki kitu kimoja ambacho yeye anaamini kuhusu Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni. Rudia hivi mpaka kila mtoto amepata nafasi ya kushiriki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Makala ya Imani

Mimi ninaamini katika injili ya Yesu Kristo.

Unaweza kutumia Makala ya Imani ili kufanyia marejeo na watoto baadhi ya imani za msingi za Kanisa la Yesu Kristo. Je, kwa nini ni muhimu kwamba watoto unaowafundisha waamini katika kweli hizi rahisi?

Shughuli Yamkini

  • Chagua makala chache za imani ambazo unahisi zina umuhimu mahususi kwa watoto unaowafundisha. Kwa kila makala ya imani, onesha picha (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii) au hadithi (kutoka kwenye maandiko au maisha yako mwenyewe) ambayo inaelezea au kufafanua ukweli unaofundishwa katika makala hiyo. Waambie watoto kwa nini ukweli huo ni muhimu kwako wewe, na acha nao waeleze kwa nini ni muhimu kwao.

  • Tafuta nyimbo za kanisa au nyimbo za watoto ambazo zinaweza kuwasaidia watoto kuelewa moja au zaidi ya makala hizi za imani. Pengine watoto wanaweza kukusaidia kuchagua. Imbeni nyimbo hizi pamoja, na wasaidie watoto kuona jinsi nyimbo hizo zinavyohusiana na makala hizi za imani.

Makala ya Imani 1:9; Matamko Rasmi 1 na 2

Bwana analiongoza Kanisa Lake kupitia nabii Wake.

Wakati waumini wa Kanisa wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali, sisi tunaweza kupata amani katika kujua kwamba Baba wa Mbinguni yuko tayari kutupa ufunuo ili kutuongoza. Wasaidie watoto unaowafundisha kuimarisha imani yao kwamba Mungu analiongoza Kanisa kupitia nabii anayeishi.

mvulana akiangalia mkutano mkuu

Baba wa Mbinguni hutuongoza kupitia manabii.

Shughuli Yamkini

  • Onesha seti ya maandiko na picha ya nabii anayeishi (au toleo la mkutano mkuu wa hivi karibuni la Ensign au Liahona). Wasaidie watoto kuamua kitu gani kinahusiana na kifungu cha maneno “yote Mungu aliyoyafunua” na kitu gani kinahusiana na kifungu cha maneno “yote ambayo sasa anayafunua” (Makala ya Imani 1:9).

  • Zima taa, na weka picha ya Yesu Kristo ubaoni. Mulika tochi ilipo picha ili kuonesha namna nabii, kama ilivyo tochi, anavyotusaidia sisi kumwona Mwokozi kwa uwazi zaidi.

  • Tafuta maelekezo rahisi ya kutengeneza kitu fulani, kama vile chakula au mwanasesere. Fuata maelekezo hayo pamoja na watoto, na elezea kwamba kupitia nabii, Baba wa Mbinguni anatupa maelekezo ili kutusaidia sisi kurudi kuishi pamoja Naye. Je, ni baadhi ya mambo gani nabii ametufundisha sisi ili tuweze kurudi kwa Mungu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Makala ya Imani

Makala za Imani zinatufundisha kweli rahisi za injili.

Nyakati zingine injili inaweza kuonekana kubwa na yenye kutatiza, hususani kwa watoto. Makala za Imani zinaweza kuwasaidia watoto kuelewa, katika njia iliyo rahisi, baadhi ya kweli za msingi tunazoamini kama Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike kila mtoto kuchagua neno muhimu au kifungu cha maneno kutoka katika makala mojawapo ya imani na kukishiriki na darasa. Kisha acha watoto wengine wabahatishe (au watafute) neno au kifungu hicho kimetoka kwenye makala ipi ya imani . Waombe watoto kueleza kwa nini neno au kifungu walichochagua ni muhimu.

  • Siku chache kabla, waombe watoto wachache kujitayarisha kushiriki darasani ujumbe mfupi kuhusu makala ya imani waipendayo. Ujumbe wao unaweza kujumuisha picha, wimbo, hadithi au uzoefu, au maandiko mengine. Waalike watoto hawa kuelezea kwa nini wamependa makala hiyo ya imani waliyoichagua.

  • Andika ubaoni maswali ambayo baadhi ya watu wanaweza kuwa nayo kuhusu imani yetu ambayo yanaweza kujibiwa na moja ya makala ya imani. Waombe watoto kuchagua swali na kutafuta makala ya imani inayojibu swali hilo. Waache wafanye mazoezi ya kujibu swali kwa kutumia makala ya imani.

Matamko Rasmi 1 na 2

Manabii hutusaidia sisi kujua mapenzi ya Baba wa Mbinguni.

Matamko Rasmi 1 na 2 ni mifano bora ya jinsi manabii wanavyopokea na kutendea kazi ufunuo kutoka kwa Mungu. Je, utawasaidiaje watoto kuongeza imani yao kwamba Mungu analiongoza Kanisa Lake kwa ufunuo?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kutafuta makala ya imani ambayo inafundisha kuhusu manabii au ufunuo. Waalike kuelezea kwa nini wana shukrani kwa ajili ya kuwa na nabii anayeishi. Shiriki baadhi ya mifano ya jinsi ambavyo Mungu ameliongoza Kanisa kupitia ufunuo, ikijumuisha mifano iliyoelezewa katika Matamko Rasmi 1 na 2, na acha watoto washiriki mifano wanayoielewa wao (kama vile mabadiliko ya hivi karibuni katika programu au sera za Kanisa).

  • Wapatie watoto marejeleo yafuatayo ya maandiko: 2 Nefi 26:33; Yakobo 2:27. Waalike kuamua andiko lipi linahusiana na Tamko Rasmi 1 (ambalo lilisababisha mwisho wa ndoa za wake wengi) na lipi linahusiana na Tamko Rasmi 2 (ambalo lilifanya baraka za ukuhani na za hekaluni zipatikane kwa watu wa jamii zote). Toa ushuhuda wako kwamba Bwana hufunua mapenzi Yake kwa manabii wa kale na wa sasa.

  • Andika yafuatayo kutoka Tamko Rasmi 1 ubaoni: “mtaamua ninyi wenyewe.” Inamaanisha nini kuamua sisi wenyewe wakati nabii anapopokea ufunuo? Ili kuwasaidia kujibu swali hili, ungeweza kushiriki maelezo haya kutoka kwa Rais Russel M. Nelson: “Unaweza kujua wewe mwenyewe kile kilicho cha kweli na kile kisicho cha kweli kwa kujifunza kutambua minon’gono ya Roho” (“The Love and Laws of God” [ibada ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, Sept. 17, 2019], 4, speeches.byu.edu).

  • Chora au onesha picha ya dunia ubaoni. Mwalike mmoja wa watoto kusoma aya mbili za mwisho za barua ya Urais wa Kwanza iliyoandikwa Juni 8, 1978 ambayo imenukuliwa katika Tamko Rasmi 2 (akianza na “Yeye amesikia sala zetu …”). Waombe watoto wengine kuhesabu ni mara ngapi neno “baraka” limeonekana. Ni baraka zipi huja kutokana na injili? Waalike watoto kuziorodhesha ubaoni kuzunguka mchoro au picha ya dunia. Toa ushuhuda wako kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote ulimwenguni kote na anataka kuwabariki kwa injili Yake.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kuchagua makala ya imani watakayoikariri, na wasaidie kutengeneza mpango wa kufanya hivyo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanapenda kushiriki kile wanachojifunza. Ingawa ni wadogo, watoto wanaweza kuimarisha imani ya wanafamilia wao. Wahimize watoto kushirikiana na familia zao kitu walichojifunza katika darasa la Msingi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.)